Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya kwa wanajamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
No Thumbnail Available
Date
2025-07-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Eastern Africa Journal of Kiswahili
Abstract
Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa
katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza
madhara yake yalivyosawiriwa katika mapambano dhidi ya mihadarati
kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya
Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na McLuhan’s (1964). Muundo wa
kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika. Mbinu ya ukusanyaji data
iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo. Mwongozo wa uchanganuzi wa
yaliyomo ulitumika kukusanya data mtandaoni. Umma lengwa ulihusisha
nyimbo za kizazi kipya na mtandao. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi
ilitumika kuchagua nyimbo za kizazi kipya za Kiswahili, suala la dawa za
kulevya na mtandao wa You Tube. Kisha, usampulishaji wa kitabaka ulitumika
kuainisha nyimbo kidhima na kwa kurejelea aina tofauti ya mihadarati
iliyosawiriwa. Jumla ya nyimbo tano na mtandao mmoja ulilengwa. Kazi hii
ililenga kupata data ya kimaelezo iliyowasilishwa kwa kutumia maelezo ya
kifafanuzi, mijadala, mifano na dondoo. Matokeo ya kazi hii ni kwamba
nyimbo za kizazi kipya ziliangazia athari zake kwa jamii, familia na waraibu
wa dawa tofauti za kulevya kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii katika
mapambano dhidi ya mihadarati. Makala haya yanapendekeza mitandao
mbalimbali tofauti na ule wa YouTube kutafitiwa kwa kurejelea madhara ya
mihadarati. Pili, uchunguzi wa athari ya uraibu wa mihadarati kwa kurejelea
nyimbo nyinginezo mbali na zile za kizazi kipya. Hatimaye, madhara ya
mihadarati pia yatafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile
vichekesho, filamu na vipindi vya runinga
Description
Journal Article
Keywords
mapambano, mihadarati, mtandao, Athari, nyimbo za kizazi kipya
Citation
Ndinyo, S. M., Mohochi, E. S., & Musungu, J. J. (2025). Athari ya uraibu wa dawa za kulevya kwa wanajamii kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Eastern Africa journal of Kiswahili, 4 (1), 55-63. https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.764
