Kibuspace

Kibuspace is the institutional repository of Kibabii University, the repository preserves the University's research legacy and all aspects of knowledge generated by KIBU community for posterity

 

Communities in DSpace

Select a community to browse its collections.

Recent Submissions

Item
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
(East African Journal of Swahili Studies, 2023-03-06) Kipchirchir, Joachim Melly; Mohochi, Ernest Sangai
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini. Nadharia ya umilisi mawasiliano yake De ll Hymes (1966) iliongoza utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji. Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano. Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi. Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidin i wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza. Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza. Licha ya uwezo wa Kiswah ili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi. Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini .
Item
Maadhimisho ya Siku kuu ya Kiswahili Duniani: Upi mwelekeo mwafaka?
(Jarida la Kiswahili Sanifu, 2024-11-27) Miruka, Frida; Mohochi, Ernest Sangai; Ngugi, Pamela; Jagero, Juliet
Lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazozungumzwa zaidi ulimwenguni ikiwa na zaidi ya wasemaji Millioni 250. Hali hii pamoja na hadhi na dhima ya Kiswahili katika jamii mbalimbali ilipelekea shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika kikao chake cha 41 kutangaza Julai tarehe 7 kuwa siku kuu ya Kiswahili duniani. Hatua hii ilikifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kuwa na siku maalum ya kuadhimishwa. Katika maadhimisho ya tatu yaliyofanyika mwaka 2024 kote duniani, Jumuia ya Afrika mashariki kupitia Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA) iliandaa sherehe nchini Kenya kwa kushirikiana na Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi. Wadau waliohusishwa walikuwa baadhi ya wanataaluma, wapenzi wa lugha ya Kiswahili na Jamii ya Waswahili mjini Mombasa. Maadhimisho haya hata hivyo hayakuwahusisha wadau wote ambao wamechangia kuiinua lugha hii na kuipa sura ya Lugha ya Ulimwengu. Baadhi yao ni wataalamu kutoka vyuo vikuu mbalimbali, waandishi wa vitabu, wanahabari na walimu wa Kiswahili. Mipango ya kuandaa sherehe katika baadhi ya vyuo maalumu haikufua dafu huku vyuo vingine vikiadhimisha siku hii kando na sherehe iliyoandaliwa na KAKAMA. Kukifungia Kiswahili katika jamii na utamaduni wa Waswahili pia kunaishusha hadhi lugha hii kama lugha ya Ulimwengu. Swali linalozuka ni Je, pana haja ya kuweka mpango mwafaka wa kuadhimisha siku hii? Makala hii inaangazia nafasi ya Kiswahili katika jamii na kutathmini Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili kwa lengo la kupendekeza mikakati ya kuyaimarisha ili kujenga taswira ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya ulimwengu. Pendekezo kuu la Makala hii ni kuhimiza ushirikiano wa wadau wote katika maadhimisho ya Siku kuu ya Kiswahili duniani.
Item
Mabadiliko ya Itikadi za Ujinaishaji katika Jamii ya Wakuria
(Jarida la Kiswahili Sanifu, 2024-11-27) Mwikali, Roseline; Mohochi, Ernest Sangai; Ogola, James
Dunia ya leo ya kiutandawazi inawezesha mtagusano wa umma wa kimataifa kidijitali unaoendelea kushuhudia utamaduni chipukizi wa ujinaishaji unaozidi kushika kasi. Hivyo, makala hii inachanganua mabadiliko katika ruwaza za ujinaishaji yanayotokana na athariya elimu ya magharibi, dini, teknolojia, na utawala katika jamii ya Wakuria pamoja na athari zake. Wakuria ni jamii ndogo ya kundi la Wabantu wa Magharibi inayopatikana katika Kaunti ya Migori nchini Kenya kwenye ujirani na nchi ya Tanzania. Ujinaishaji ni sehemu muhimu ya maisha ya jamii ya Wakuria kwani ni utambulisho wao. Aidha, sawa na jamii nyingine zile, ujinaishaji huwa dafina ya historia yao. Nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Usemi mtazamo wa Kihistoria yao Wodak na Reisgil(2001)ilikuwadira katika uchanganuzi wa data zilizokusanywa. Data ambayo imetumika katika makala hii ilikusanywa kwa njia ya mahojiano ya ana kwa ana pamoja na majadiliano ya makundi. Idadi ya sampuli ilikuwa watu 42; wa kike 18 na wa kiume 24. Makala hii imebainisha kuwa mabadiliko ya kielimu, kiuchumi, kiteknolojia, kiutawala na kidini yamekuwa na athari kubwa kiitikadi katika ujinaishaji miongoni mwa Wakuria. Majilio ya elimu ya magharibi, uhuru wa kufanya biashara, mifumo ya kisiasa na mtagusano wa kiteknolojia umepelekea ukopaji wa majina kutoka makabila mengine nchini Kenya na ulimwenguni kote miongoni mwa jamii ya Wakuria. Hili linamaanisha kuwa itikadi za ujinsia zilizohodhiwa na kushamirishwa na majina ya kiasili ya Wakuria zinazidi kufifia kila uchao.
Item
Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass
(East African Journal of Swahili Studies, 2025-05-07) Kipchirchir, Joachim Melly; Wamalwa, Eric Walela; Mohochi, Ernest Sangai
Wakulima wengi nchini Kenya hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananch i kuhusu kilimo. Kwa sababu hiyo, juhudi nyingi zimeelekezwa katika kuwafikia wakulima ambao ni wahusika wakuu katika sekta ya kilimo ili kuwapa elimu ya kujiendeleza. Lugha ya Kinandi ni mojawapo ya lugha za kiasili ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass. Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi lugha ya Kinandi hutumika kuinua viwango vya kilimo miongoni mwa wanajamii kupitia vipindi vya runinga ya Kass. Utafiti huu ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ya McCombs na Shaw (1993). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Matokeo ya utafiti yalithibitisha kuwa lugha ya kinandi inayotumik a kuwasilisha vipindi vya kilimo iliwasaidia sana wakulima kuimarisha mapato katika kilimo. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu umuhimu wa matumizi ya lugha za kiasili katika kuinua viwango vya kilimo
Item
Mandhari katika Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni Zinazohusu Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya
(East African Journal of Swahili Studies, 2025-05-12) Ndinyo, Stephen Muyundo; Mohochi, Ernest Sangai; Musungu, Joseph Juma
Mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni miongoni mwa masuala yanayosawiriwa katika nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Katika kufanya hivyo, nyimbo hizo hutumia vipengele mbalimbali vya kisanii. Mojawapo kati ya vipengele hivyo ni mandhari, huku usukaji mzuri wa mandhari ukichangia fanaka katika uwasilishaji wa ujumbe wa nyimbo hizo. Makala haya yalichunguza mandhari katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Makala yaliongozwa na Nadharia ya Utendaji katika Fasihi Simul izi iliyoasisiwa na Wallace Bacon katika mwaka wa 1957. Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika katika makala haya. Uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data kutoka kwa video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu dawa za kulevya katika mtanda o wa YouTube ambao uliteuliwa kimaksudi. Aidha, nyimbo ziliteuliwa kimaksudi. Kisha, nyimbo hizo zilitabakishwa kidhima na kwa kurejelea aina tofauti za dawa za kulevya zinazosawiriwa. Jumla ya nyimbo 5 zilitumika. Data iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi na mijadala, mifano na dondoo kutoka kwenye uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionyesha kwamba aina mbalimbali ya mandhari yalibainika katika video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya mtandaoni. Mandhari ya klab u, nyumbani, barabarani, mjini, mtaani na yale ya wakati yalitumika katika vita dhidi ya uraibu wa dawa za kulevya katika jamii. Aina hizi za mandhari zilotoa mchango katika kuwasilisha ujumbe kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya. Utafiti unapendekeza kwam ba kuna haja ya kuchunguza mandhari kuhusiana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kurejelea aina nyinginezo za nyimbo mbali na zile za kizazi kipya. Pili, ni vyema mandhari yatafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga kwa kurejelea suala la dawa za kulevya .