Mchango wa Kinandi katika Kuihamasisha Jamii kuhusu Ustawi wa Kilimo Kupitia Vipindi vya Runinga ya KASS

dc.contributor.authorKipchirchir, Melly
dc.contributor.authorMohochi, Ernest Sangai
dc.contributor.authorWamalwa, Eric
dc.date.accessioned2026-03-06T11:48:50Z
dc.date.available2026-03-06T11:48:50Z
dc.date.issued2025-08-29
dc.descriptionJournal Article
dc.description.abstractMoja kati ya ajenda kuu za serikali ya sasa ya Kenya ni ustawi wa kilimo ambao huleta utoshelevu wa chakula na hivyo kuchangia katika kupunguza gharama ya maisha. Wakulima wengi nchini humo hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Wakati uo huo vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananchi kuhusu kilimo. Lugha ya Kinandi ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass, ni mojawapo ya lugha za kiasili nchini Kenya. Utafiti huu ulilenga kuchunguza mchango wa lugha ya Kinandi katika kuihamasisha jamii kuhusu ustawi wa kilimo kupitia vipindi vya kilimo katika runinga ya Kass. Utafiti ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano ya Hymes (1972). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Isitoshe watangazaji 9 vilevile walihusishwa. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu jinsi wanajamii huhamasishwa kuhusu ustawi wa kilimo kupitia vipindi vya kilimo katika runinga ya KASS.
dc.description.sponsorshipKIBU
dc.identifier.citationKipchirchir, M., Mohochi, E. S. & Wamalwa, E. (2025). Mchango wa Kinandi katika Kuihamasisha Jamii kuhusu Ustawi wa Kilimo Kupitia Vipindi vya Runinga ya KASS. Jarida la Kiswahili Sanifu, 2(2), pp. 1-10.
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/11274
dc.language.isoen
dc.publisherJarida la Kiswahili Sanifu
dc.relation.ispartofseries2; 2
dc.subjectUhakiki-maeneo
dc.subjectUkweli
dc.subjectBunilizi
dc.titleMchango wa Kinandi katika Kuihamasisha Jamii kuhusu Ustawi wa Kilimo Kupitia Vipindi vya Runinga ya KASS
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
JAKISA22001.pdf
Size:
375.81 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections