Mchango wa Kinandi katika Kuihamasisha Jamii kuhusu Ustawi wa Kilimo Kupitia Vipindi vya Runinga ya KASS
No Thumbnail Available
Date
2025-08-29
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Jarida la Kiswahili Sanifu
Abstract
Moja kati ya ajenda kuu za serikali ya sasa ya Kenya ni ustawi wa kilimo ambao huleta
utoshelevu wa chakula na hivyo kuchangia katika kupunguza gharama ya maisha.
Wakulima wengi nchini humo hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako
mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Wakati uo huo vyombo vya habari ni
miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za
kiasili na kuwahamasisha wananchi kuhusu kilimo. Lugha ya Kinandi ambayo hutumiwa
katika runinga ya Kass, ni mojawapo ya lugha za kiasili nchini Kenya. Utafiti huu ulilenga
kuchunguza mchango wa lugha ya Kinandi katika kuihamasisha jamii kuhusu ustawi wa
kilimo kupitia vipindi vya kilimo katika runinga ya Kass. Utafiti ulifanyika katika kaunti ya
Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano ya Hymes (1972).
Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264
walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Isitoshe watangazaji 9 vilevile walihusishwa.
Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa
vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa
maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kisha ikawasilishwa
kwa kutumia asilimia na majedwali. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa
wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu jinsi wanajamii huhamasishwa kuhusu ustawi
wa kilimo kupitia vipindi vya kilimo katika runinga ya KASS.
Description
Journal Article
Keywords
Uhakiki-maeneo, Ukweli, Bunilizi
Citation
Kipchirchir, M., Mohochi, E. S. & Wamalwa, E. (2025). Mchango wa Kinandi katika Kuihamasisha Jamii kuhusu Ustawi wa Kilimo Kupitia Vipindi vya Runinga ya KASS. Jarida la Kiswahili Sanifu, 2(2), pp. 1-10.
