Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass

dc.contributor.authorKipchirchir, Joachim Melly
dc.contributor.authorWamalwa, Eric Walela
dc.contributor.authorMohochi, Ernest Sangai
dc.date.accessioned2026-03-06T12:13:23Z
dc.date.available2026-03-06T12:13:23Z
dc.date.issued2025-05-07
dc.descriptionJournal Article
dc.description.abstractWakulima wengi nchini Kenya hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananch i kuhusu kilimo. Kwa sababu hiyo, juhudi nyingi zimeelekezwa katika kuwafikia wakulima ambao ni wahusika wakuu katika sekta ya kilimo ili kuwapa elimu ya kujiendeleza. Lugha ya Kinandi ni mojawapo ya lugha za kiasili ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass. Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi lugha ya Kinandi hutumika kuinua viwango vya kilimo miongoni mwa wanajamii kupitia vipindi vya runinga ya Kass. Utafiti huu ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ya McCombs na Shaw (1993). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Matokeo ya utafiti yalithibitisha kuwa lugha ya kinandi inayotumik a kuwasilisha vipindi vya kilimo iliwasaidia sana wakulima kuimarisha mapato katika kilimo. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu umuhimu wa matumizi ya lugha za kiasili katika kuinua viwango vya kilimo
dc.description.sponsorshipKIBU
dc.identifier.citationJoachim , M . K . , Wamalwa , E. W . & Mohochi , S . (202 5 ). Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass . East African Journal of Swahili Studies , 8 ( 1 ), 3 01 - 3 13 . https://doi.org/10.37284/ jammk . 8 . 1 . 2 9 5 8
dc.identifier.issn2707 - 3467 | 2707 - 3475
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/11278
dc.language.isoen
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studies
dc.relation.ispartofseries8; 1
dc.subjectLugha
dc.subjectKinandi
dc.subjectRuninga
dc.subjectKilimo
dc.subjectWakulima
dc.titleMatumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
2958-Article Text-8102-2-10-20250506.pdf
Size:
339.92 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections