Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass
No Thumbnail Available
Date
2025-05-07
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Wakulima wengi nchini Kenya hupatikana katika maeneo ya mashambani
ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Vyombo vya habari
ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi
ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananch
i kuhusu kilimo. Kwa sababu
hiyo, juhudi nyingi zimeelekezwa katika kuwafikia wakulima ambao ni
wahusika wakuu katika sekta ya kilimo ili kuwapa elimu ya kujiendeleza.
Lugha ya Kinandi ni mojawapo ya lugha za kiasili ambayo hutumiwa katika
runinga ya Kass.
Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi lugha ya Kinandi
hutumika kuinua viwango vya kilimo miongoni mwa wanajamii kupitia vipindi
vya runinga ya Kass. Utafiti huu ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa
na Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ya McCombs
na Shaw (1993).
Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264
walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Mbinu za hojaji, uchunzaji na
mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya
data ni: mwongozo
wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya
mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia
lengo la utafiti kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali.
Matokeo ya utafiti yalithibitisha kuwa lugha ya kinandi inayotumik
a
kuwasilisha vipindi vya kilimo iliwasaidia sana wakulima kuimarisha mapato
katika kilimo. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa
kuwa ulitoa mwanga kuhusu umuhimu wa matumizi ya lugha za kiasili katika
kuinua viwango vya kilimo
Description
Journal Article
Keywords
Lugha, Kinandi, Runinga, Kilimo, Wakulima
Citation
Joachim , M . K . , Wamalwa , E. W . & Mohochi , S . (202 5 ). Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass . East African Journal of Swahili Studies , 8 ( 1 ), 3 01 - 3 13 . https://doi.org/10.37284/ jammk . 8 . 1 . 2 9 5 8
