Department of Kiswahili and Other African Languages
Permanent URI for this collectionhttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/100
Browse
Recent Submissions
Item Language of Instruction under the Competency-based Curriculum of Kenya: Policy, Practice and Performance(The International Journal of Humanities and Social Studies, 2021-11-01) Odeo, Isaac Ipara; Ongeti, Karren Ohanga; Abenga, ElizabethIn Kenya, the educational language policy stipulates that the language of instruction in lower primary Grade 1 to 3 in rural settings should be the learners’ First Language or Mother Tongue. In urban settings, the language of the school’s catchment area (usually English or Kiswahili) should be used as the language of instruction in Grade 1 to 3. Kiswahili and English are to be taught as subjects. English becomes the medium of instruction in all settings from Grade 4 onwards. This policy creates problems for teachers and learners considering that Kenya is linguistically heterogeneous. The purpose of this study was to establish the actual language practice in lower primary school Grade 1 to 3 in relation to declared policy and to evaluate its relationship with learners’ academic achievement. The objectives of the study were to establish the actual status of educational language policy and language practice in lower primary schools; to assess the relationship between the language of instruction and English subject scores of learners at Grade 4; to assess the relationship between the language of instruction and Mathematics subject scores of learners at Grade 4. The study area was Kakamega County, which was selected based on being a county with a fair mix of urban, rural and semi-urban schools. The study adopted a correlational design. The study population comprised 1,120 primary schools and 10,767 Grade 4 learners. Multistage sampling was used to select a sample of 175 schools from the population. Questionnaires were administered to 75 teachers and mean scores of Grade 4 assessment results were obtained from 1,076 learners from the sampled schools as part of a different, larger study. The data were analysed using descriptive statistics. Inferential statistics were used to test the hypotheses. The findings of the study indicate that there is a gap between policy and practice in lower primary school. The study revealed that there is a strong correlation between the language of instruction at lower primary school and learners’ academic achievement at Grade 4 in English and in Mathematics subjects. A policy shift is recommended to unify the language of instructions in the new CBC framework. This is imperative for equality of outcome in the learners’ Grade 4 school-based assessment under the CBCItem Hadithi fupi_utanzu uliopuuzwa(1997) Mohochi, Ernest SangaiItem The role of creative arts in the fight against COVID-19 in Kenya(East African Scholars Publisher, Kenya, 2021-02-01) Mohochi, Ernest Sangai; Mwita, James MarwaInitial response to the outbreak and fast spread of the coronavirus (Covid-19) disease was very slow in most countries. Rightly, most efforts at understanding it turned to and concentrated on the medical field, and within a very short time, its economic impact gained a central place in ensuing discussions on the pandemic. Little attention was given to non-health related aspects like the social and psychological implications, the role of religious and other traditional believe systems in understanding and combating Covid-19. Even less thought was given to contribution of the latter factors and others in efforts at fighting its wide spread and measure at containing it. This paper takes the position that fighting the Covid-19 disease needs to be multifaceted in order to present a holistic affront on the dangers it possesses. The paper argues that creative artists have a key role to play in this fight and uses examples from Kenya to indicate that role. It discusses works of artists from different genres of literature, and brings their contribution to the fore. Aspects like the presentation of the pandemic, messages contained, and language used in weaving their art are looked at and their role presented. It concludes that creative artists‘ role in society clearly goes beyond entertainment and calls for them to be included in various initiatives, spanning all sectors including sustainable development efforts and health related campaignsItem Mielekeo ya Lugha na Ruwaza za Matumizi ya Lugha ya walimu wa Kiswahiliwa shule za msingi(KIBU, 2020-01) Wamalwa, Eric Walela; Mohochi, Ernest Sangai; Odeo, Isaac IparaMielekeo ni moja kati ya dhana za taaluma ya sayansi-tabia iliyoshughulikiwa na watafiti kwa zaidi ya karne moja iliyopita. Mielekeo imefanyiwa uchunguzi mwingi na matokeo yake kuchapishwa katika taaluma za saikolojia, isimujamii na saikolojia jamii ya lugha (Kircheri, 2010). Kwa kuwa tafiti hizo zilifanywa kwa misingi ya taaluma mbalimbali, hakuna fasili ya moja kwa moja ya mielekeo. Hata hivyo, fasili zifuatazo zitaufaidi uchunguzi huu.Item Signification of HIV/AIDS in Babu Omar’s Kala Tufaha(KIBU, 2016-06) Kinara, Gladys; Muindu, JaphethPopular fiction takes literary ideas to the masses and ‘is meant to fulfill the spiritual enjoyment of all, it preaches values of equality and material wellbeing for all’ (Wanjala, 214).As a subgenre of popular fiction, Kenyan AIDS novels play a didactic role and are a useful literary intervention against a life threatening illness. Examples of AIDS themed novels in Kenya includeCarolyne Adalla’s Confessions of an AIDS Victim (1993), Meja Mwangi’s The Last Plague (2000), Wahome Mutahi’s The House of Doom (2004), Francis Imbuga’s Miracle of Remera (2004), Joseph Situma’s The Mysterious Killer (2001), and Moraa Gitaa’s Cruciblefor Silver and Furnacefor Gold (2008). Kenyan prose fiction written in Kiswahili has also made a significant contribution in representing AIDS. Babu Omar’s Kala Tufaha (2004) and William Mkufya’s Ua La Faraja(2005) are exemplary in their literary representation of the pandemic. While the novels written in English have received commensurate critical attention, for instance, (Muindu, 2014), there is a dearth of critical interpretation of the Kiswahili texts.The paper is an analysis of Babu Omar’s Kala Tufaha which takes as its central problem the significations AIDS in the novel. The examination of these significations through Judith Butler’s concept of linguistic performativity, where discourses bring into being what they name, offers fresh insight into novelistic interventions against AIDS. The paper appropriates Butler’s concepts to the discursive formation of illness identities and the construction of the diseased corporeality in discourse. It enriches the understanding of the function of the novel in fostering better conceptualization of the illness and it is a modest contribution to the existing scholarly interpretation of AIDS novels in Kenya.Item Matumizi ya Maigizo kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenya(KIBU, 2019-08-23) Misiko, David Wasike; Simbi, Inviolata Wekesa; Amukowa, Deborah Wanyama; Masinde, EdwinUtafiti huu ulilenga kuonyesha matumizi ya maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia; mfano wa Kigogo katika shule za upili, Kaunti ya Bungoma Kusini. Ufundishaji wa somo lolote hujikita kwenye mawasiliano baina ya mwalimu na mwanafunzi. Mbinu za kufundisha huwa viungo muhimu vya kufanikisha mawasiliano haya. Mwalimu ana jukumu la kuteua mbinu mwafaka ya kufundisha. Kuna mbinu mbalimbali mwalimu anaweza kutumia kufundisha tamthilia. Utafiti huu umechagua maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza iwapo walimu wanatumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia na wanatumia kwa jinsi gani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utendaji inayoshikilia kuwa matini ya kidrama huwasilisha ujumbe vyema zaidi kupitia uigizaji wake katika jukwaa. Utafiti ulilenga shule kumi na sita kati ya shule hamsini na mbili. Walimu wanaofundisha Kiswahili kidato cha tatu na nne pamoja na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne ndio waliolengwa. Watafitiwa waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya utabakishaji, kinasibu na usampulishaji kimaksudi. Stadi ya utabakishaji ilitumika kuainisha shule katika makundi matatu. Mbinu ya kimaksudi ilitumika kuteua shule tatu za kaunti na walimu wanaofundisha kiswahili kidato cha tatu na nne. Mbinu ya kinasibu ilitumika kuteua shule za kaunti ndogo, shule kumi na mbili na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Wanafunzi kumi katika kila kidato waliteuliwa, jumla ya wanafunzi mia tatu ishirini walitafitiwa. mbinu zlizotumika kukusanya data zilikuwa hojaji, maswali ya usaili na uchunzaji. Maswali ya usaili yalitumika kukusanya data kutoka kwa walimu. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia maelezo, asilimia, picha na majedwali. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kuwa walimu 83% ndio walitumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia ya Kigogo. Utafiti unapendekeza kuwa mbinu za maigizo ambazo hazitumiki pia zitumike ili kuboresha ufundishaji. Vile vile taasisi ya elimu kuandaa semina na warsha za kuwahamasisha walimu kuhusu njia mbalimbali za kutumia maigizo kufundisha. Aidha kila shule iwe na klabu cha maigizo ili kutumika katika ufundishaji wakati wowote.Item Dhima ya Mwingilianotanzu katika Sherehe za Mwaka Kogwa(KIBU, 2018-01-01) Simiyu, Fred WanjalaMakala hii inahusu umuhimu wa mwingilianotanzu katika fasihi simulizi ya Kiafrika kwa kutumia mfano wa miviga ya mwaka kogwa. Utafiti ulitumia miviga ya mwaka kogwa kama mfano wa jukwaa linalotoa fursa ya kudhihirisha mwingilianotanzu katika fasihi simulizi ya Kiafrika. Madhumuni ya makala hii ni kuonyesha namna ambavyo mwingilianotanzu huamilisha miviga ya mwaka kogwa. Imebainika kuwa, miviga ya mwaka kogwa hujengwa na kuamilishwa kutokana na uchanganyikaji wa tanzu zinazoingiliana kikorasi na kimatini, kutenguana, kujinyambua na kusemezana wakati wa utendaji. Mahusiano haya kati ya tanzu hizi ndani ya mwaka kogwa husaidia miviga hii kutekeleza wajibu wake kupitia njia anuai. Matokeo ya utafiti huu yamethibitisha maoni ya Senkoro (2011), aliyedai kuwa, inawezekana kabisa kuwa, tanzu za fasihi simulizi hazipaswi kuainishwa moja moja. Utafiti ulifanywa katika kisiwa cha Zanzibar na uchanganuzi ukafanywa kwa mujibu wa malengo ya utafiti. Mbinu ya Uchunzaji-Mahuluti inayojumuisha kushiriki, kushuhudia na kuhoji ilitumika katika kukusanya nyimbo, majigambo, malumbano ya utani na maghani, zikiwa tanzu kuu zilizowasilishwa wakati wa sherehe za Mwaka Kogwa, mwaka wa 2016. Kimsingi, utafiti huu umethibitisha kuwa, miviga ya mwaka kogwa ni mfumo timilifu wa maarifa, ambao unajengwa kutokana na mchanganyiko wa tanzu na vipera visivyoweza kutenganishwa katika hali halisi ya utendaji. Mchanganyiko huu wa tanzu ndio huiwezesha kutekeleza majumu yake mbalimbali miongoni mwa Wamakunduchi. Haya ni kinyume na mkabala uliopo unaopania kutenganisha fasihi simulizi katika tanzu zinazojitegemea (Bayo 2012, Okporoboro 2006, Ogumbiyi 1988 na Kubik 1977). Kwa hivyo, utafiti huu unaboresha mbinu za uainishaji na uchanganuzi wa fasihi simulizi ya Kiafrika kwa kuzingatia sifa ya mwingilianotanzu.Item Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka(KIBU, 2020-07-15) Simiyu, Fred Wanjala; Adero, Margan; Chepkwony, JoyceUtafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo. Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo. Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka. Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972. Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga. Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini. Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School. Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70. Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa. Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.Item Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu(KIBU, 2020-12-01) Simiyu, Fred Wanjala; Wekesa, Winnie Musailo; Opande, Nilson IsaacUtafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.Item Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria(KIBU, 2020-08-13) Simiyu, Fred Wanjala; Wekesa, Winnie Musailo; Opande, Nilson IsaacUtafiti ulilenga kubainisha vipengele maalum vya Fasihi Simulizi vinavyooana na hali katika taaluma ya Sheria. Utafiti uliegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano ya utafiti. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha michakato miwili ya uteuzi wa sampuli; ikiwa ni uteuzi sampuli kimaksudi na kinasibu. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tulioyahudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaji kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.Item The Role of Language in Facilitating Culture: A Case Study of the Isukha Community, Kakamega County in Kenya(KIBU, 2019-09-06) Simiyu, Fred Wanjala; Kibigo, Mary Lukamika; Choge, Susan ChebetThe study explores the role of language specifically nouns in portraying masculinity in the Isukha culture during the ritual of Shilembe and the indigenous sport of Mayo. Culture is the way of life of a people. A people’s culture is encompassed in their language. Thus, it is not possible to delink the Isukha language from their culture especially through the praise poetry that is chanted by the artists during bullfighting. The Isukha community from Shinyalu Sub County of Kakamega County, Kenya, participates in bullfighting as a ritual known as Shilembe. This ritual involves two bulls fighting on the grave of a male hero who has died but while alive he killed either a wild animal or an enemy of the community. They also participate in bullfighting as an indigenous sport that is referred to as Mayo. However, the study discovered that the two games are not just done as a ritual and an indigenous sport respectively during bullfighting but rather the praise poems that are chanted possess language aspects that portray masculinity. The study used Hegemonic Masculinity and Critical Discourse Analysis to analyse the language used by the artists in the praise poems. The findings of this study will be helpful in understanding African communities like the Isukha, especially when it comes to male chauvinism.Item A Critical Discourse Analysis of Linguistic and Discursive Strategies Used in Kenya’s Citizen Television Advertisements to Display Gender Ideologies(KIBU, 2020-10-14) Simiyu, Fred Wanjala; Mayoyo, Edna Magoma; Khaemba, JosephineThe present study sought to examine how linguistic devices and discursive strategies used in Kenya’s Citizen TV ads which pattern men and women differently according to gender well-being. This thereby results in unconscious rationalisations of social constructions. Using observation as the main tool of data collection, a corpus of fourteen adverts sourced from one mainstream media station, Citizen TV were purposively sampled, observed by the researcher, transcribed into data, coded, then thematically analysed using techniques of content analysis. Guided by Fairclough’s Critical Discourse Analysis theory which provided the framework for analysis, the study adopted a qualitative, case study research design. The research design provided in-depth information about the phenomenon in order to establish the discursive and linguistic strategies used in the TV ads and how they mirror society’s system of values, attitudes and beliefs about men and women. The findings of this study indicated that gender ideologies that affect how meaning is made out of Kenyan TV ads were embedded in linguistic structures, social processes and manoeuvres.Item Masimulizi katika mchakato wa ufundishaji wa kipengele maalum cha msuko katika riwaya ya kidagaa kimemwozea na ile ya chozi la heri(Eanso, 2019-08-23) Ndinyo, Stephen Muyundo; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, DeborahMasimulizi katika mchakato wa ufundishaji wa vipengele maaalum vya msuko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri. Lengo la Makala haya lilikuwa ni kubainisha namna ambavyo masimulizi yalivyojitokeza katika mchakato wa ufundishaji wa kipengele maalum cha msuko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri. Utafiti huu ulitumia muundo wa kithamano mkabala wa kimfano. Mbinu za ukusanyaji data zilizotumiwa ni uchunzaji usaili na majadiliano ya vikundi viini. Data iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi ,majedwali, nukuu za dondoo kutoka kwa mahojiano. Sampuli lengwa ilihusisha shule 10 kati ya 27, wasailiwa 18 kati ya 54 katika Kaunti ndogo ya Navakholo. Matokeo ni kwamba matukio yalitiririshwa katika mchakato wa ufundishaji wa vipengele maalum vya fani na maudhui katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri.Item Mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini kenya(Eanso, 2019-08-23) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, DeborahUtafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji na uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu hasa ulilenga kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kudhihirisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundishia uainishaji wa nyimbo darasani na kuonesha namna ambavyo uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki huzisaidia nyimbo husika kutekeleza wajibu wake. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ufundishaji wa fasihi simulizi lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake unakanganya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu inayoonesha utaratibu wa kuainisha fasihi katika misingi ya aina mbalimbali kwa kuegemea miundo na maumbo, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii ambayo inashikilia kuwa ujifunzaji ni mchakato wa utambuzi ambao hujitokeza katika muktadha wa kijamii. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya. Kauli mbiu yake ilikuwa kuboresha umoja wa kitaifa kwa kuunganisha na kuleta watu pamoja. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu na ya kimakusudi. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano na picha. Mtafiti alipata kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulibaini kuwa, tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi darasani. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wanaItem Mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya(Easo, 2019-08-23) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, DeborahUtafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji na uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu hasa ulilenga kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kudhihirisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundishia uainishaji wa nyimbo darasani na kuonesha namna ambavyo uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki huzisaidia nyimbo husika kutekeleza wajibu wake. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ufundishaji wa fasihi simulizi lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake unakanganya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu inayoonesha utaratibu wa kuainisha fasihi katika misingi ya aina mbalimbali kwa kuegemea miundo na maumbo, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii ambayo inashikilia kuwa ujifunzaji ni mchakato wa utambuzi ambao hujitokeza katika muktadha wa kijamii. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya. Kauli mbiu yake ilikuwa kuboresha umoja wa kitaifa kwa kuunganisha na kuleta watu pamoja. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu na ya kimakusudi. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano na picha. Mtafiti alipata kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulibaini kuwa, tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi darasani. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wanafunzi na walimu katika ufundishaji wa nyimbo kama kipera cha fasihi simulizi.Item Dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa wanandi(Easo, 2019-11-15) Koech, Jenniffer Chepleting; Simiyu, Fred Wanjala; Adero, MarganWakenya wengi hushutumu suala la umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za wasanii maarufu nchini. Madai yao ni kuwa umahuluti wa utamaduni husababisha kupotea kwa utamaduni asili wa jamii mbalimbali za Wakenya na kuiga ule wa Wakoloni. Utafiti huu ulikusudia kuhakiki dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wanandi nchini Kenya. Nadharia ambayo iliongoza utafiti huu ni ya ubaada ukoloni. Baadhi ya wahasisi wakuu wa nadharia hii ni Homi Bhabha, Gayatri Chakravorty Spinak, Edward Said, Robert Young na Bill Ashcroft. Mtafiti alipata data yake kupitia usaili na uchanganuzi wa yaliyomo kwenye vipindi vya Tumdo katika runinga ya Kass. Jumla ya wahojiwa nane walisailiwa kutoka kata ya Chepsaita, eneo la kaunti ndogo ya Turbo kwenye kaunti ya Uasin-Gishu. Idadi kubwa ya wakazi wa Uasin-Gishu ni Wanandi ambao walihamia eneo hilo kutoka kaunti ya Nandi; kwa hivyo wameingiliana na jamii zingine wa hapa nchini na kimataifa. Sampuli tajwa ilitumiwa kuteua wasailiwa. Nadharia ya ubaada ukoloni iliwaongoza mtafiti kubainisha vipengele vya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi. Hatimaye data iliyokusanywa iliwasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa: Nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kwenye runinga ya Kass zina vipengele vingi vya utamaduni wa jadi katika jamii ya Wanandi. Vilevile, nyimbo hizo zina baadhi ya vipengele vigeni hasa vinavyochangiwa na teknolojia na mwingiliano baina ya Wanandi na jamii zingine. Kadhalika umahuluti wa utamaduni umesaidia nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kutekeleza majukumu yake katika jamii ya sasa. Kwa hivyo, utafiti huu ni muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi na vyombo vya habari hasa kwa wale walimu na wanafunzi watakaotaka kufanya utafiti wa suala la dhima ya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi kwenye jamii za kiafrika.Item Tamathali za semi zinazosawiri ubabedume katika majigambo ya miviga ya shilembe na mchezasili wa mayo ya waisukha, nchini kenya kwa mtazamo wa semantiki(East African nature & science organization, 2019-09-06) Lukamika, Mary Kibigo; Choge, Susan Chebet; Simiyu, Fred WanjalaMakala hii imewasilisha baadhi ya matokeo ya utafiti wa Uzamifu uliotafitia ubabedume katika majigambo ya miviga ya Shilembe na mchezasili wa Mayo katika jamii ya Waisukha nchini Kenya kwa mtazamo wa semantiki. Utafiti huu ulihakiki tamathali mbalimbali za semi ambazo ni chuku, jazanda na majazi miongoni mwa nyingine kwa kutumia mtazamo wa kisemantiki ili kudhihirisha namna zinavyosawiri ubabedume katika miviga ya Shilembe na Mchezasili wa Mayo. Utafiti huu ulifanyika katika Kaunti Ndogo ya Shinyalu, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ya kwanza ni nadharia ya Uwezo-Uume iliyoasisiwa na Robert Bly na kuendelezwa na Izugbara. Inahusu mahusiano ya wanaume na wanawake katika jamii. Nadharia ya pili iliyotumiwa ni ile ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi (UCHAMAWADI). Nadharia hii ina misingi yake katika kazi mbalimbali za wataalam tofauti ulimwenguni. Nadharia mbili zilitumiwa ili kuoanisha taaluma ya Fasihi na Isimu. Utafiti huu ulitumia majigambo kumi na sita kwa kutumia uchunzaji-shiriki, dodoso, unasaji sauti na ujazaji wa hojaji. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa lugha ya majigambo inayoghaniwa na fanani hubeba tamathali za semi zinazosawiri ubabedume. Hivyo, sherehe hizi zitumiwe kama jukwaa la kuelimisha vizazi vichanga vya jamii hii kuhusu mila na desturi zao. Utafiti huu umeonyesha kuwa Fasihi Simulizi ya Mwafrika ni hai. Utafiti umegundua kuwa, lugha ni kipengele muhimu katika jamii. Hata hivyo, utafiti umetambua kuwa, wakati mwingine lugha hutumiwa vibaya na wanajamii kumtukuza Mwanamume kupita kiasi na kumpa uwezo na mamlaka dhidi ya mwanamke. Isitoshe, ubabedume umejengwa katika mila, itikadi na utamaduni wa jamii husika. Makala hii imeweka wazi baadhi ya matokeo ya utafiti huu.Item Lugha kama rasilimali ya jamii: uchunguzi wa redio za fm zinazotumia kibukusu katika kaunti ya bungoma(Moi University, 2017-01-12) Misiko, David WasikeMatumizi ya lugha za kiasili yameshutumiwa na watu wengi kwa kukuza ukabila haswa nchini Kenya. Hata hivyo, lugha hizi zinaweza kuwa rasilimali kwa wazungumzaji zikitumiwa vyema. Utafiti huu ulilenga kuchunguza lugha za kiasili zinavyojitokeza kama rasilimali kwa wazungumzaji wake zinapotumika katika redio za FM. Aidha, utafiti ulinuia kujadili jinsi matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yanavyowezesha jamii husika kupata habari zinazoziwezesha kuboresha hali zao za maisha kwa njia mbalimbali. Uchunguzi ulidhamiria hususan: Kuhakiki yaliyomo katika vipindi vya jamii, uchumi, siasa na afya vinavyowasilishwa kwa kutumia Kibukusu katika redio za FM, zinazosikika katika kaunti ya Bungoma; Kutathmini Kibukusu kinavyojitokeza kama rasilimali kuangazia masuala ya jamii, uchumi, siasa na afya kwa wazungumzaji wake kinapotumika katika redio za FM, kisha kutambua changamoto za matumizi ya Kibukusu kama rasilimali kwa wakaazi wa Bungoma kupitia vituo vya redio za FM. Utafiti ulitumia mbinu za ustahilivu na kikiasi. Lahaja ya Kibukusu ilitafitiwa katika mazingira halisi ambapo lugha hiyo hutumika na wazungumzaji wake. Miktadha ya matumizi ya Kibukusu ilichunguzwa, hususan kama rasilimali kwa wazungumzaji wake. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili; Sarufi Amilifu ya Halliday na ya Uanzilishi wa Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Show. Sarufi Amilifu ilihusishwa katika uchanganuzi wa vipindi vinavyopeperushwa kwa kutumia lugha za kiasili. Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa vipindi vinavyopeperushwa na vituo hivyo viwili vya redio. Uchunguzi ulifanywa katika vituo vya Sulwe na West FM vinavyopeperusha matangazo kwa Kibukusu katika kaunti ya Bungoma. Utafiti ulihusisha mhariri mmoja, watangazaji wawili na wataalamu wanne; mmoja kwa kila mojawapo ya masuala haya; jamii, uchumi, afya na siasa ambao hualikwa kwa kila mojawapo ya vituo hivyo. Vilevile, wasikilizaji 70 kutoka kila mojawapo ya vituo hivyo viwili vya redio walihusishwa. Kwa jumla, utafiti uliwahusisha watu 154. Wasikilizaji hao waliteuliwa kutoka kwa kaunti ndogo sita za kaunti ya Bungoma na walihusisha jinsia zote. Wasikilizaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimakusudi ambao huwezesha idadi ya wahojiwa kuongezeka kadiri utafiti unavyoendelea. Vipindi vya redio vya vituo vyote viwili vilivyohusiana na masuala ya jamii, afya, uchumi na siasa vilisikilizwa. Mbinu ya ujazaji wa hojaji kwa watangazaji na wasikilizaji, usaili wa wahariri, watangazaji na wataalamu na kurekodi vipindi mahususi zilitumika. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa wanahabari, hohaji kwa wasikilizaji, mwongozo wa usaili kwa wahariri, watangazaji na wataalamu na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sarufi Amilifu. Data ifuatayo ilikusanywa: vipindi vya redio vinavyotumia lahaja ya Kibukusu, yaliyomo katika vipindi hivyo, Kibukusu kinavyojitokeza kama rasilimali kwa wazungumzaji wake na changamoto za matumizi ya lahaja hiyo katika redio za FM. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kwa maelezo na takwimu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa yafuatayo: Matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yalijaza pengo liliokuwepo katika upashaji habari kwa watu walioko mashinani; Matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yaliwezesha wazungumzaji kufikia maamuzi faafu kuhusiana na masuala ya afya, siasa, uchumi na jamii; ukosefu wa taasisi ya kudhibiti uundaji wa istilahi ni mojawapo ya changamoto zinazokumba matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM. Matokeo ya utafiti huu yalitoa picha halisi ya mchango wa lugha za kiasili katika redio za FM nchini Kenya kwa maendeleo ya jamii husika. Matokeo ya uchunguzi huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu matumizi ya lugha za Kiafrika katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utawafaidi wapangaji lugha kitaifa na katika viwango vya kaunti. Utafiti huu pia unatarajiwa kutoa mchango kwa uhifadhi na makuzi ya lugha za Kiafrika kichanya. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Kuundwa kwa taasisi za kutafiti, kuunda na kudhibiti istilahi zinazotumika katika lugha za kiasili; Vyuo vikuu kufundisha baadhi ya lugha hizi za kiasili ili kubadilisha mtazamo hasi kuzihusu; Serikali za kaunti kuanzisha sera za lugha katika viwango vya kaunti na hatimaye, kufufuliwa kwa ufundishaji wa lugha za kiasili mbali na Kiingereza, Kiswahili na lugha zingine za kigeni kama vile Kifaransa na Kijerumani katika sera ya lugha nchini Kenya.Item Baker’s strategies in translation: a lexico-semantic analysis of four luhya dialects; Lukabras, Lwisukha, Luwanga and Lukhayo in informative text(KIBU, 2018-09-03) Angatia, Mudogo BenardThere exist numerous strategies of dealing with the problem of Target Language Non-equivalence in the translation of different text types. In this regard, Baker’s proposed strategies for dealing with nonequivalence at the word level have been widely discussed in translation studies. Yet, no studies have ever applied her strategies simultaneously for describing and assessing the functional appropriateness in translating informative texts. This study is an attempt to compare the word-level translation strategies used in an informative text type, based on Baker’s suggested strategies for attaining Target Language Equivalence at the word level. Mulembe FM newscasts being an informative text, was selected for analysis. The main question is whether the translators’ word-level strategies used to attain functional Target Language equivalence in Mulembe FM newscasts can be described and assessed by Baker’s framework or not. To do so, some pre-recorded transcripts from the Luhya Mulembe FM newscasts broadcast by Lukhayo, Luwanga and Lwisukha presenters were selected, and then, they were compared with their corresponding functional equivalent versions of Lukabras listeners. Then, comparisons were classified and analyzed in terms of translating using a superordinate word, using loan word plus explanations, substitution, and using a specific word to find out which strategies were used, and to show the extent of the Target Language functional equivalence in the translation of the newscasts by the presenters. The investigation was motivated by the fact that although the Luhya dialects exhibit vast lexical mismatches, Mulembe FM hiring policy is that the presenters use their dialects in the newscast translation on the assumption that the dialects are mutually intelligible. The study focuses on Lukabras listeners as representatives of Luhya listeners who have to be accommodated in the newscasts. The results showed that Bakers’s procedures are nearly comprehensive and worked well for describing and assessing the translation of informative text.Item Challenges of teaching the revised Kiswahili syllabus in secondary schools, a case study of Bungoma west district Kenya(KIBU, 2018-09-03) Molenje, Mary L.The purpose of this study was to find out the challenges facing the teaching of the revised syllabus of Kiswahili in secondary schools in Bungoma West District. The performance of Kiswahili language dropped in the recent years after the revision of the syllabus, (KNEC, 2007, 2008). The objective of the study was to establish teacher preparedness in teaching the revised Kiswahili syllabus. The study was based on Krashen’s input hypothesis and affective filter theory which is relevant to the study. A descriptive survey research design was adopted. The study targeted secondary schools in Bungoma West District. Purposive sampling was used to get the respondents from 6 schools of the 18 secondary schools in the district. Simple random sampling was used to select 6 Head teachers, 6 Kiswahili teachers and 300 form three students. Data was collected using questionnaires and interview schedules. The data was analyzed using descriptive statistics where frequency distribution tables and percentages. The findings revealed that 22.2% of the teachers in Bungoma West district have diploma qualification, 33.3% of the teachers have a Bachelor degree, and 44.4% of the teachers were untrained. With regard to in-service training 16.67% of teachers often received in-service training on the teaching of the revised Kiswahili syllabus. Teachers who had not received in-service training “quite often” were 50% while 33.33% of the teachers had never received inservice training on the revised Kiswahili syllabus. On how often teachers received in-service training, 11.11% of the teachers had received in service training often while 33.33% had received in service training “less often”, and 55.56% had not received any in service training at all on the teaching of the revised Kiswahili syllabus. On the issue of professional records, 16.7% of teachers prepared their professional records on time, 33.3% of the teachers didn’t prepare their professional record on time and 50% of teachers at times prepare their professional records on time.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »
