Itikadi za Ujinsia katika Maumbo ya Majina ya Kikuria
No Thumbnail Available
Date
2023-03-11
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Ruwaza Afrika
Abstract
Majina ni vipengele vya lugha ambavyo hutaja mtu, kitu, hali, mahali, dhana na tendo na
huweza kufunua itikadi na matukio katika maisha ya wanajamii. Itikadi ni mawazo
ambayo humwongoza kila mtu ulimwenguni katika kutenda anayotenda na hivyo
kuhalalisha au kuharamisha matendo anayoyafanya. Makala haya yanajikita katika
kuchanganua jinsi maumbo ya majina ya Kikuria katika jamii ya Wakuria iliyoko nchini
Kenya hushamirisha itikadi za ujinsia. Itikadi za ujinsia ni imani, mielekeo na mitazamo
inayoongoza jamii kuhusu mgawanyo wa majukumu kwa kuangalia jinsia. Lengo kuu la
makala haya ni kuainisha jinsi maumbo ya majina ya Kikuria hudumisha na kuendeleza
itikadi za ujinsia. Data iliyotumika katika makala haya ilikusanywa kwa njia ya
mahojiano ya ana kwa ana na majadiliano ya makundi. Ukusanyaji na uchanganuzi wa
data uliongozwa na Nadharia ya Onomastiki. Nadharia hii imekuwa dira katika
kubainisha maumbo ya majina ya Wakuria na jinsi maumbo haya huakisi itikadi za
ujinsia katika jamii ya Wakuria. Utafiti wetu uliweza kubainisha kuwa vipo vipashio
ambavyo hudokeza jinsia na shughuli inayohusishwa nazo au nafasi yake katika jamii.
Kwa misingi hii, utafiti wetu ulibainisha kuwa jinsia ya kiume kwa mujibu wa majina yao
yaliyoteuliwa kiitikadi, ilitengewa shughuli na nafasi zilizoikweza ikilinganishwa na
jinsia ya kike.
Description
Journal Article
Keywords
Itikadi za Ujinsia, Maumbo, Majina, Shughuli, Wakuria
Citation
Kasuma , R, Ogola, J., & Mohochi, E. S. (2023). Itikadi za Ujinsia katika Maumbo ya Majina ya Kikuria. Ruwaza Afrika, 2(1), pp. 20-30.
