Athari za Dhana Potofu Kuhusu Afrika na Mwafrika Kwa Jamii ya Waafrika Kama Zinavyodhihirishwa Katika Riwaya Teule za Euphrase Kezilahab
No Thumbnail Available
Date
2021-11-26
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
CHAKITA
Abstract
Suala la dhana potofu kuhusu Afrika na Mwafrika lina historia ndefu sana. Historia yake inaweza kutazamwa kuanzia kipindi cha ukoloni. Dhana hizo potofu kuhusu Afrika na Mwafrika zilijengewa msingi wake sio tu katika vitabu vya dini kama vile Biblia Takatifu, bali pia kwa wanafalsafa na wasomi maarufu wa kale wa Kimagharibi kama vile Carl Meinhof na Georg Hegel. Dhana potofu zilizopandikizwa zilichochea kutawaliwa kwa Waafrika na Afrika kwa jumla. Kwa mfano, kwa kupitia Biblia Takatifu kuna hoja kuwa masaibu, shida, majanga na mambo mbalimbali yanayomsibu Mwafrika yanatokana na kulaaniwa. Kutokana na kuwapo kwa dhana potofu, makala hii inakusudia kutathmini mikakati mbalimbali inayopendekezwa na Euphrase Kezilahabi katika kukabiliana na dhana hizo. Mikakati hiyo itabainishwa kupitia riwaya za Kezilahabi za Gamba la Nyoka, Nagona na Mzingile. Aidha, katika kubainisha dhana hizo, tutaongozwa na baadhi ya mihimili ya Nadharia ya Ubaadaukoloni. Hii ni Nadharia inayofungamanishwa na Edward Said hususani baada ya kuandika kitabu chake cha Orientalism (1978).
Description
Journal Article
Keywords
Dhana Potovu, Afrika, Euphrase Kezilahab
