Uasi au Utatu katika Ujitambulishaji wa Wanajenizi: Matumizi ya Mihadarati katika Nyimbo za Gengetone

dc.contributor.authorSimiyu, Fred, C. N. W.
dc.date.accessioned2026-03-20T06:09:39Z
dc.date.available2026-03-20T06:09:39Z
dc.date.issued2026-03-17
dc.descriptionJournal Article
dc.description.abstractMakala hii inahusu matumizi ya uasi ndani ya utatu kama mkakati wa kutambulisha vijana wa Jenizi kupitia nyimbo za Gengetone. Fasihi simulizi kupitia kipera kimojawapo cha nyimbo za gengetone, inatumiwa kupinga na au kuhimiza matumizi ya mihadarati kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali. Kwa jicho la haraka, inaonekana kuwa, baadhi ya waimbaji wa gengetone wanashabikiwa ukiukaji wa ukawaida wa kijami. Hata hvivo, kwa kutumia jicho la ndani, imebainika kuwa, wasanii hawa wanapinga mifumo dhalimu ya kijamii na kupendekeza mwamko mpya. Kwa hivyo, ni muhimu kuchanganua nyimbo teule za gengetone kwa jicho la ndani ili kubainisha kiini chake. Kutokana na haya, makala hii inachunguza mikakati inayotumiwa kuasi ukawaida, matumizi ya uasi kama silka ya ujitambulishaji; na matumizi ya utatu kama mkakati wa kupinga unyanyaswaji wa wanyonge kupitia nyimbo za gengetone. Haya yamebainishwa katika makala haya, ambapo uchambuzi wa nyimbo tano za gengetone umefanywa kwa kuongozwa na Nadharia ya Utatu. Uchambuzi wa data katika makala hii umedhihirisha kwamba nyimbo za Gengetone zinakua kwa kasi kikubwa sana kutokana na uwezo wake wa kujinyambua, ili kupanua mipaka yake. Ujinyambuaji huu unafanywa kwa kuchopeka mitindo mipya ili kuendelea kuwa hai, kuvutia na kusisimua. Isitoshe, Gengetone siyo tu aina ya muziki, bali ni aina maalum ya ujitambulishaji wa vijana wa mjini. Huu ni mfano mzuri wa nguvu za sanaa zinazotumiwa kuvunja kuta za ukabila, kuunganisha tamaduni mbalimbali, na kutoa jukwaa la kuwawezesha vijana kutoa sauti zao. Ni jukwaa la utatu ambalo linaloonesha ukakamavu, ubunifu na uzalendo wa vijana wa mjini.
dc.description.sponsorshipKIBU
dc.identifier.citationSimiyu, F. C. N. W. (2026). Uasi au Utatu katika Ujitambulishaji wa Wanajenizi: Matumizi ya Mihadarati katika Nyimbo za Gengetone. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 4(1), 24- 34.
dc.identifier.issn2958-4914
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/11457
dc.language.isoen
dc.publisherJournal of Kiswahili and Other African Languages
dc.relation.ispartofseries4; 1
dc.subjectJenizi
dc.subjectMihadarati
dc.subjectUasi
dc.subjectUtatu
dc.titleUasi au Utatu katika Ujitambulishaji wa Wanajenizi: Matumizi ya Mihadarati katika Nyimbo za Gengetone
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Dr Sim Uasi au Utatu katika Ujitambulishaji wa Wanajenizi Article 2026.pdf
Size:
275.6 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections