Maadhimisho ya Siku kuu ya Kiswahili Duniani: Upi mwelekeo mwafaka?
No Thumbnail Available
Date
2024-11-27
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Jarida la Kiswahili Sanifu
Abstract
Lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazozungumzwa zaidi ulimwenguni
ikiwa na zaidi ya wasemaji Millioni 250. Hali hii pamoja na hadhi na dhima ya Kiswahili
katika jamii mbalimbali ilipelekea shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) katika kikao chake cha 41 kutangaza Julai tarehe 7 kuwa siku kuu
ya Kiswahili duniani. Hatua hii ilikifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika
kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kuwa na siku maalum ya kuadhimishwa. Katika
maadhimisho ya tatu yaliyofanyika mwaka 2024 kote duniani, Jumuia ya Afrika mashariki
kupitia Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA) iliandaa sherehe nchini Kenya
kwa kushirikiana na Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi. Wadau waliohusishwa
walikuwa baadhi ya wanataaluma, wapenzi wa lugha ya Kiswahili na Jamii ya Waswahili
mjini Mombasa. Maadhimisho haya hata hivyo hayakuwahusisha wadau wote ambao
wamechangia kuiinua lugha hii na kuipa sura ya Lugha ya Ulimwengu. Baadhi yao ni
wataalamu kutoka vyuo vikuu mbalimbali, waandishi wa vitabu, wanahabari na walimu
wa Kiswahili. Mipango ya kuandaa sherehe katika baadhi ya vyuo maalumu haikufua dafu
huku vyuo vingine vikiadhimisha siku hii kando na sherehe iliyoandaliwa na KAKAMA.
Kukifungia Kiswahili katika jamii na utamaduni wa Waswahili pia kunaishusha hadhi lugha
hii kama lugha ya Ulimwengu. Swali linalozuka ni Je, pana haja ya kuweka mpango
mwafaka wa kuadhimisha siku hii? Makala hii inaangazia nafasi ya Kiswahili katika jamii
na kutathmini Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili kwa lengo la kupendekeza mikakati ya
kuyaimarisha ili kujenga taswira ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya ulimwengu.
Pendekezo kuu la Makala hii ni kuhimiza ushirikiano wa wadau wote katika maadhimisho
ya Siku kuu ya Kiswahili duniani.
Description
Journal Article
Keywords
Nyimbo, Kiswahili, Utamaduni, Siku kuu ya Kiswahili, Lugha ya Kimataifa, Ushirikiano
Citation
Frida M., Ernest M., Pamela N., & Juliet J.(2024). Maadhimisho ya siku kuu ya kiswahili duniani: Upi mwelekeo mwafaka?Jarida la Kiswahili Sanifu 1(2024), 33–40
