Mandhari katika Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni Zinazohusu Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya
No Thumbnail Available
Date
2025-05-12
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni miongoni mwa masuala
yanayosawiriwa katika nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Katika kufanya
hivyo, nyimbo hizo hutumia vipengele mbalimbali vya kisanii. Mojawapo kati
ya vipengele hivyo ni mandhari, huku usukaji mzuri
wa mandhari ukichangia
fanaka katika uwasilishaji wa ujumbe wa nyimbo hizo. Makala haya
yalichunguza mandhari katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kupitia
nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Makala yaliongozwa na Nadharia ya
Utendaji katika Fasihi Simul
izi iliyoasisiwa na Wallace Bacon katika mwaka
wa 1957. Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika katika
makala haya. Uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data kutoka kwa
video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu dawa za kulevya katika mtanda
o wa
YouTube ambao uliteuliwa kimaksudi. Aidha, nyimbo ziliteuliwa kimaksudi.
Kisha, nyimbo hizo zilitabakishwa kidhima na kwa kurejelea aina tofauti za
dawa za kulevya zinazosawiriwa. Jumla ya nyimbo 5 zilitumika. Data
iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya
kifafanuzi na mijadala, mifano na
dondoo kutoka kwenye uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionyesha
kwamba aina mbalimbali ya mandhari yalibainika katika video za nyimbo za
kizazi kipya kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya mtandaoni.
Mandhari ya klab
u, nyumbani, barabarani, mjini, mtaani na yale ya wakati
yalitumika katika vita dhidi ya uraibu wa dawa za kulevya katika jamii. Aina
hizi za mandhari zilotoa mchango katika kuwasilisha ujumbe kuhusu vita dhidi
ya dawa za kulevya. Utafiti unapendekeza kwam
ba kuna haja ya kuchunguza
mandhari kuhusiana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kurejelea
aina nyinginezo za nyimbo mbali na zile za kizazi kipya. Pili, ni vyema
mandhari yatafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho,
filamu
na vipindi vya runinga kwa kurejelea suala la dawa za kulevya
.
Description
Journal Article
Keywords
Mandhari, Mapambano, Nyimbo za kizazi Kipya, Mtandaoni na Dawa za Kulevya
Citation
Ndinyo , S . M . , Mohochi , E. S . & Musungu , J. J . (202 5 ). Mandhari katika Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni Zinazohusu Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya . East African Journal of Swahili Studies , 8 ( 1 ), 3 14 - 3 26 . https://doi.org/10.37284/ jammk . 8 . 1 . 2 9 8 3
