Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria

dc.contributor.authorWekesa, Winnie Musailo
dc.contributor.authorSimiyu, Fred Wanjala
dc.contributor.authorOpande, Nilson Isaac
dc.date.accessioned2026-06-10T06:47:25Z
dc.date.available2026-06-10T06:47:25Z
dc.date.issued2020-06-10
dc.descriptionJournal Article
dc.description.abstractUtafiti ulilenga kubainisha vipengele maalum vya Fasihi Simulizi vinavyooana na hali katika taaluma ya Sheria. Utafiti uliegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano ya utafiti. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha michakato miwili ya uteuzi wa sampuli; ikiwa ni uteuzi sampuli kimaksudi na kinasibu. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tulioyahudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaji kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.
dc.description.sponsorshipKIBU
dc.identifier.citationWekesa, W., Simiyu, F., & Opande, N. (2020). Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria. East African Journal of Swahili Studies, 2(2), 65-83. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.193
dc.identifier.issn2707-3467
dc.identifier.issn2707-3475
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/11836
dc.language.isoen
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studies
dc.relation.ispartofseries2; 2
dc.subjectVipengele
dc.subjectFasihi Simulizi
dc.subjectTaaluma
dc.subjectSheria.
dc.titleVipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
193-Article Text-489-1-10-20200813_compressed.pdf
Size:
203.96 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections