Browsing by Author "Musungu, Joseph Juma"
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya kwa wanajamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni(Eastern Africa Journal of Kiswahili, 2025-07-06) Ndinyo, Stephen Muyundo; Mohochi, Ernest Sangai; Musungu, Joseph JumaSuala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawiriwa katika mapambano dhidi ya mihadarati kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na McLuhan’s (1964). Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika. Mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo. Mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data mtandaoni. Umma lengwa ulihusisha nyimbo za kizazi kipya na mtandao. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika kuchagua nyimbo za kizazi kipya za Kiswahili, suala la dawa za kulevya na mtandao wa You Tube. Kisha, usampulishaji wa kitabaka ulitumika kuainisha nyimbo kidhima na kwa kurejelea aina tofauti ya mihadarati iliyosawiriwa. Jumla ya nyimbo tano na mtandao mmoja ulilengwa. Kazi hii ililenga kupata data ya kimaelezo iliyowasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi, mijadala, mifano na dondoo. Matokeo ya kazi hii ni kwamba nyimbo za kizazi kipya ziliangazia athari zake kwa jamii, familia na waraibu wa dawa tofauti za kulevya kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii katika mapambano dhidi ya mihadarati. Makala haya yanapendekeza mitandao mbalimbali tofauti na ule wa YouTube kutafitiwa kwa kurejelea madhara ya mihadarati. Pili, uchunguzi wa athari ya uraibu wa mihadarati kwa kurejelea nyimbo nyinginezo mbali na zile za kizazi kipya. Hatimaye, madhara ya mihadarati pia yatafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runingaItem Mandhari katika Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni Zinazohusu Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya(East African Journal of Swahili Studies, 2025-05-12) Ndinyo, Stephen Muyundo; Mohochi, Ernest Sangai; Musungu, Joseph JumaMapambano dhidi ya dawa za kulevya ni miongoni mwa masuala yanayosawiriwa katika nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Katika kufanya hivyo, nyimbo hizo hutumia vipengele mbalimbali vya kisanii. Mojawapo kati ya vipengele hivyo ni mandhari, huku usukaji mzuri wa mandhari ukichangia fanaka katika uwasilishaji wa ujumbe wa nyimbo hizo. Makala haya yalichunguza mandhari katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Makala yaliongozwa na Nadharia ya Utendaji katika Fasihi Simul izi iliyoasisiwa na Wallace Bacon katika mwaka wa 1957. Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika katika makala haya. Uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data kutoka kwa video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu dawa za kulevya katika mtanda o wa YouTube ambao uliteuliwa kimaksudi. Aidha, nyimbo ziliteuliwa kimaksudi. Kisha, nyimbo hizo zilitabakishwa kidhima na kwa kurejelea aina tofauti za dawa za kulevya zinazosawiriwa. Jumla ya nyimbo 5 zilitumika. Data iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi na mijadala, mifano na dondoo kutoka kwenye uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionyesha kwamba aina mbalimbali ya mandhari yalibainika katika video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya mtandaoni. Mandhari ya klab u, nyumbani, barabarani, mjini, mtaani na yale ya wakati yalitumika katika vita dhidi ya uraibu wa dawa za kulevya katika jamii. Aina hizi za mandhari zilotoa mchango katika kuwasilisha ujumbe kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya. Utafiti unapendekeza kwam ba kuna haja ya kuchunguza mandhari kuhusiana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kurejelea aina nyinginezo za nyimbo mbali na zile za kizazi kipya. Pili, ni vyema mandhari yatafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga kwa kurejelea suala la dawa za kulevya .
