Browsing by Author "Kipchirchir, Joachim Melly"
Now showing 1 - 3 of 3
- Results Per Page
- Sort Options
Item Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo(East African Journal of Swahili Studies, 2023-03-06) Kipchirchir, Joachim Melly; Mohochi, Ernest SangaiUtafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini. Nadharia ya umilisi mawasiliano yake De ll Hymes (1966) iliongoza utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji. Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano. Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi. Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidin i wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza. Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza. Licha ya uwezo wa Kiswah ili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi. Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini .Item Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass(East African Journal of Swahili Studies, 2025-05-07) Kipchirchir, Joachim Melly; Wamalwa, Eric Walela; Mohochi, Ernest SangaiWakulima wengi nchini Kenya hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananch i kuhusu kilimo. Kwa sababu hiyo, juhudi nyingi zimeelekezwa katika kuwafikia wakulima ambao ni wahusika wakuu katika sekta ya kilimo ili kuwapa elimu ya kujiendeleza. Lugha ya Kinandi ni mojawapo ya lugha za kiasili ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass. Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi lugha ya Kinandi hutumika kuinua viwango vya kilimo miongoni mwa wanajamii kupitia vipindi vya runinga ya Kass. Utafiti huu ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ya McCombs na Shaw (1993). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Matokeo ya utafiti yalithibitisha kuwa lugha ya kinandi inayotumik a kuwasilisha vipindi vya kilimo iliwasaidia sana wakulima kuimarisha mapato katika kilimo. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu umuhimu wa matumizi ya lugha za kiasili katika kuinua viwango vya kilimoItem Uimarishaji wa Lugha za Kiasili Kupitia Vyombo vya Habari: Mfano wa Kinandi katika Runinga ya Kass(Editon Consortium Journal of Kiswahili, 2025-07-07) Kipchirchir, Joachim Melly; Wamalwa, Eric Walela; Mohochi, Ernest SangaiLugha za kiasili ni muhimu sana katika kufanikisha mawasiliano kwa kuwa hutumiwa na watu wengi. Hata hivyo lugha hizi zinapitia changamoto kwa kuwa idadi ya wazungumzaji inazidi kupunguka. Hii ni kwa sababu lugha hizi zinapuuzwa huku lugha za Kiswahili na Kingereza zikitukuzwa. Hali hii inawafanya watu wengi kutumia Kiswahili katika mawasiliano ya mara kwa mara. Kutokana na umuhimu wa lugha za kiasili, ipo haja ya kuziimarisha. Makala hii inafafanua jinsi vipindi vya kilimo katika runinga ya Kass vinachangia katika uimarishaji wa lugha ya Kinandi. Uchunguzi uliozaa makala hii ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Mawasiliano ya Sperka (1966). Washiriki 264 waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika uchunguzi. Mbinu za hojaji, utazamaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Data zilikusanywa kwa kutumia mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kitakwimu na kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha zikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Kutokana na uchunguzi huu, tumetambua kuwa lugha ya Kinandi inaweza kuimarishwa kupitia njia zifuatazo: Kuhimiza matumizi ya Kinandi katika mawasiliano ya mara kwa mara, kuwafundisha watoto kama lugha ya kwanza, kuifundisha shuleni kama mojawapo ya masomo, kuhimiza matumizi katika vyombo vya habari na kuhifadhi kwenye maandishi.
