Tamathali za semi zinazosawiri ubabedume katika majigambo ya miviga ya shilembe na mchezasili wa mayo ya waisukha, nchini kenya kwa mtazamo wa semantiki
Date
2019-09-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African nature & science organization
Abstract
Makala hii imewasilisha baadhi ya matokeo ya utafiti wa Uzamifu uliotafitia
ubabedume katika majigambo ya miviga ya Shilembe na mchezasili wa Mayo
katika jamii ya Waisukha nchini Kenya kwa mtazamo wa semantiki. Utafiti huu
ulihakiki tamathali mbalimbali za semi ambazo ni chuku, jazanda na majazi
miongoni mwa nyingine kwa kutumia mtazamo wa kisemantiki ili kudhihirisha
namna zinavyosawiri ubabedume katika miviga ya Shilembe na Mchezasili wa
Mayo. Utafiti huu ulifanyika katika Kaunti Ndogo ya Shinyalu, Kaunti ya
Kakamega, nchini Kenya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ya kwanza
ni nadharia ya Uwezo-Uume iliyoasisiwa na Robert Bly na kuendelezwa na
Izugbara. Inahusu mahusiano ya wanaume na wanawake katika jamii. Nadharia
ya pili iliyotumiwa ni ile ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi
(UCHAMAWADI). Nadharia hii ina misingi yake katika kazi mbalimbali za
wataalam tofauti ulimwenguni. Nadharia mbili zilitumiwa ili kuoanisha taaluma
ya Fasihi na Isimu. Utafiti huu ulitumia majigambo kumi na sita kwa kutumia
uchunzaji-shiriki, dodoso, unasaji sauti na ujazaji wa hojaji. Matokeo ya utafiti
yalionyesha kuwa lugha ya majigambo inayoghaniwa na fanani hubeba
tamathali za semi zinazosawiri ubabedume. Hivyo, sherehe hizi zitumiwe kama
jukwaa la kuelimisha vizazi vichanga vya jamii hii kuhusu mila na desturi zao.
Utafiti huu umeonyesha kuwa Fasihi Simulizi ya Mwafrika ni hai. Utafiti
umegundua kuwa, lugha ni kipengele muhimu katika jamii. Hata hivyo, utafiti
umetambua kuwa, wakati mwingine lugha hutumiwa vibaya na wanajamii
kumtukuza Mwanamume kupita kiasi na kumpa uwezo na mamlaka dhidi ya
mwanamke. Isitoshe, ubabedume umejengwa katika mila, itikadi na utamaduni
wa jamii husika. Makala hii imeweka wazi baadhi ya matokeo ya utafiti huu.
Description
Keywords
Ubabedume, Upiganishaji Fahali, Majigambo, Shilembe, Mayo