Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Wamalwa, Eric Walela"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 2 of 2
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Matumizi ya Lugha ya Kinandi katika Kuendeleza Kilimo kupitia Vipindi vya Runinga ya Kass
    (East African Journal of Swahili Studies, 2025-05-07) Kipchirchir, Joachim Melly; Wamalwa, Eric Walela; Mohochi, Ernest Sangai
    Wakulima wengi nchini Kenya hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananch i kuhusu kilimo. Kwa sababu hiyo, juhudi nyingi zimeelekezwa katika kuwafikia wakulima ambao ni wahusika wakuu katika sekta ya kilimo ili kuwapa elimu ya kujiendeleza. Lugha ya Kinandi ni mojawapo ya lugha za kiasili ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass. Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi lugha ya Kinandi hutumika kuinua viwango vya kilimo miongoni mwa wanajamii kupitia vipindi vya runinga ya Kass. Utafiti huu ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ya McCombs na Shaw (1993). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Matokeo ya utafiti yalithibitisha kuwa lugha ya kinandi inayotumik a kuwasilisha vipindi vya kilimo iliwasaidia sana wakulima kuimarisha mapato katika kilimo. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu umuhimu wa matumizi ya lugha za kiasili katika kuinua viwango vya kilimo
  • No Thumbnail Available
    Item
    Uimarishaji wa Lugha za Kiasili Kupitia Vyombo vya Habari: Mfano wa Kinandi katika Runinga ya Kass
    (Editon Consortium Journal of Kiswahili, 2025-07-07) Kipchirchir, Joachim Melly; Wamalwa, Eric Walela; Mohochi, Ernest Sangai
    Lugha za kiasili ni muhimu sana katika kufanikisha mawasiliano kwa kuwa hutumiwa na watu wengi. Hata hivyo lugha hizi zinapitia changamoto kwa kuwa idadi ya wazungumzaji inazidi kupunguka. Hii ni kwa sababu lugha hizi zinapuuzwa huku lugha za Kiswahili na Kingereza zikitukuzwa. Hali hii inawafanya watu wengi kutumia Kiswahili katika mawasiliano ya mara kwa mara. Kutokana na umuhimu wa lugha za kiasili, ipo haja ya kuziimarisha. Makala hii inafafanua jinsi vipindi vya kilimo katika runinga ya Kass vinachangia katika uimarishaji wa lugha ya Kinandi. Uchunguzi uliozaa makala hii ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Mawasiliano ya Sperka (1966). Washiriki 264 waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika uchunguzi. Mbinu za hojaji, utazamaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Data zilikusanywa kwa kutumia mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kitakwimu na kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha zikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Kutokana na uchunguzi huu, tumetambua kuwa lugha ya Kinandi inaweza kuimarishwa kupitia njia zifuatazo: Kuhimiza matumizi ya Kinandi katika mawasiliano ya mara kwa mara, kuwafundisha watoto kama lugha ya kwanza, kuifundisha shuleni kama mojawapo ya masomo, kuhimiza matumizi katika vyombo vya habari na kuhifadhi kwenye maandishi.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback