Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Simiyu, Fred Wanjala"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 20 of 26
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    A Critical Discourse Analysis of Linguistic and Discursive Strategies Used in Kenya’s Citizen Television Advertisements to Display Gender Ideologies
    (East African Journal of Arts and Social Sciences, 2020-10-14) Mayoyo, Edna Magoma; Khaemba, Josephine; Simiyu, Fred Wanjala
    The present study sought to examine how linguistic devices and discursive strategies used in Kenya’s Citizen TV ads which pattern men and women differently according to gender well-being. This thereby results in unconscious rationalisations of social constructions. Using observation as the main tool of data collection, a corpus of fourteen adverts sourced from one mainstream media station, Citizen TV were purposively sampled, observed by the researcher, transcribed into data, coded, then thematically analysed using techniques of content analysis. Guided by Fairclough’s Critical Discourse Analysis theory which provided the framework for analysis, the study adopted a qualitative, case study research design. The research design provided in-depth information about the phenomenon in order to establish the discursive and linguistic strategies used in the TV ads and how they mirror society’s system of values, attitudes and beliefs about men and women. The findings of this study indicated that gender ideologies that affect how meaning is made out of Kenyan TV ads were embedded in linguistic structures, social processes and manoeuvres.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    A Critical Discourse Analysis of Linguistic and Discursive Strategies Used in Kenya’s Citizen Television Advertisements to Display Gender Ideologies
    (KIBU, 2020-10-14) Simiyu, Fred Wanjala; Mayoyo, Edna Magoma; Khaemba, Josephine
    The present study sought to examine how linguistic devices and discursive strategies used in Kenya’s Citizen TV ads which pattern men and women differently according to gender well-being. This thereby results in unconscious rationalisations of social constructions. Using observation as the main tool of data collection, a corpus of fourteen adverts sourced from one mainstream media station, Citizen TV were purposively sampled, observed by the researcher, transcribed into data, coded, then thematically analysed using techniques of content analysis. Guided by Fairclough’s Critical Discourse Analysis theory which provided the framework for analysis, the study adopted a qualitative, case study research design. The research design provided in-depth information about the phenomenon in order to establish the discursive and linguistic strategies used in the TV ads and how they mirror society’s system of values, attitudes and beliefs about men and women. The findings of this study indicated that gender ideologies that affect how meaning is made out of Kenyan TV ads were embedded in linguistic structures, social processes and manoeuvres.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Dhima ya Futuhitandao Katika Kukabiliana na Masuala ya Afya ya Akili Miongoni Mwa Wakenya
    (Eastern Africa Journal of Kiswahili, 2025-06-09) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Orina, Felix Ayioka
    Fasihi kupitia utambuzi na tanzu zake tofauti tofauti, tangu jadi, imekuwa na majukumu mahususi ya kutekeleza katika jamii. Kama utanzu mojawapo wa fasihi simulizi, futuhi imetumika pakubwa katika vyombo vya habari kama vile televisheni na redioni kuwafurahisha na kuwachekesha watazamaji na wasikilizaji. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, futuhi imechukua mkondo tofauti katika uwasilishaji wake. Hii ni kwa sababu ya njia mpya ya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa ambayo imezua mitandao ya kijamii kama vile Facebook, TikTok, Twitter, Instagram na YouTube. Mbinu mpya za kiteknolojia sasa zipo kwa wingi kuliko wakati mwingine wowote. Licha ya mkurupuko wa mbinu hizi, tusisahau kwamba tangu jadi futuhi imekuwa muhimu katika jamii mbalimbali. Lakini sasa futuhi imekuwa karibu zaidi kwa sababu ya teknolojia ya kisasa. Vile vile, suala la afya ya akili limekuwa nyeti miongoni mwa Wakenya. Hivyo basi, kukawa na haja ya kuchunguza zaidi kuhusu futuhi katika mitandao hii ya kijamii na afya ya akili miongoni mwa Wakenya. Mada hii vile vile ilichaguliwa kwa sababu tafiti ambazo zilihusu futuhi, ziliegemea futuhi katika vitabu vya riwaya na tamthilia na hazikujikita katika suala la afya ya akili. Hivyo basi, makala haya yalinuia kujaza pengo hili kwa kutafitia futuhitandao na afya ya akili miongoni mwa Wakenya, na hasa kwa kuzingatia futuhi zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebook, Twitter na YouTube. Makala haya yalitumia nadharia ya Burudiko ya Sigmund Freud. Utafiti huu ulitumia muundo wa kiethnografia, mkabala wa kithamano. Data kuhusu futuhitandao ilikusanywa kwa mbinu ya Uchanganuzi wa Yaliyomo. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimakusudi na kinasibu. Umuhimu wa makala haya ni kuwa, matokeo yake yatasaidia katika ufundishaji wa futuhi. Inapendekezwa kuwa tafiti zaidi zifanywe kuhusu suala la afya ya akili kwa kurejelea vipera vingine vya fasihi simulizi.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Dhima ya Mwingilianotanzu katika Sherehe za Mwaka Kogwa
    (KIBU, 2018-01-01) Simiyu, Fred Wanjala
    Makala hii inahusu umuhimu wa mwingilianotanzu katika fasihi simulizi ya Kiafrika kwa kutumia mfano wa miviga ya mwaka kogwa. Utafiti ulitumia miviga ya mwaka kogwa kama mfano wa jukwaa linalotoa fursa ya kudhihirisha mwingilianotanzu katika fasihi simulizi ya Kiafrika. Madhumuni ya makala hii ni kuonyesha namna ambavyo mwingilianotanzu huamilisha miviga ya mwaka kogwa. Imebainika kuwa, miviga ya mwaka kogwa hujengwa na kuamilishwa kutokana na uchanganyikaji wa tanzu zinazoingiliana kikorasi na kimatini, kutenguana, kujinyambua na kusemezana wakati wa utendaji. Mahusiano haya kati ya tanzu hizi ndani ya mwaka kogwa husaidia miviga hii kutekeleza wajibu wake kupitia njia anuai. Matokeo ya utafiti huu yamethibitisha maoni ya Senkoro (2011), aliyedai kuwa, inawezekana kabisa kuwa, tanzu za fasihi simulizi hazipaswi kuainishwa moja moja. Utafiti ulifanywa katika kisiwa cha Zanzibar na uchanganuzi ukafanywa kwa mujibu wa malengo ya utafiti. Mbinu ya Uchunzaji-Mahuluti inayojumuisha kushiriki, kushuhudia na kuhoji ilitumika katika kukusanya nyimbo, majigambo, malumbano ya utani na maghani, zikiwa tanzu kuu zilizowasilishwa wakati wa sherehe za Mwaka Kogwa, mwaka wa 2016. Kimsingi, utafiti huu umethibitisha kuwa, miviga ya mwaka kogwa ni mfumo timilifu wa maarifa, ambao unajengwa kutokana na mchanganyiko wa tanzu na vipera visivyoweza kutenganishwa katika hali halisi ya utendaji. Mchanganyiko huu wa tanzu ndio huiwezesha kutekeleza majumu yake mbalimbali miongoni mwa Wamakunduchi. Haya ni kinyume na mkabala uliopo unaopania kutenganisha fasihi simulizi katika tanzu zinazojitegemea (Bayo 2012, Okporoboro 2006, Ogumbiyi 1988 na Kubik 1977). Kwa hivyo, utafiti huu unaboresha mbinu za uainishaji na uchanganuzi wa fasihi simulizi ya Kiafrika kwa kuzingatia sifa ya mwingilianotanzu.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa wanandi
    (Easo, 2019-11-15) Koech, Jenniffer Chepleting; Simiyu, Fred Wanjala; Adero, Margan
    Wakenya wengi hushutumu suala la umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za wasanii maarufu nchini. Madai yao ni kuwa umahuluti wa utamaduni husababisha kupotea kwa utamaduni asili wa jamii mbalimbali za Wakenya na kuiga ule wa Wakoloni. Utafiti huu ulikusudia kuhakiki dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wanandi nchini Kenya. Nadharia ambayo iliongoza utafiti huu ni ya ubaada ukoloni. Baadhi ya wahasisi wakuu wa nadharia hii ni Homi Bhabha, Gayatri Chakravorty Spinak, Edward Said, Robert Young na Bill Ashcroft. Mtafiti alipata data yake kupitia usaili na uchanganuzi wa yaliyomo kwenye vipindi vya Tumdo katika runinga ya Kass. Jumla ya wahojiwa nane walisailiwa kutoka kata ya Chepsaita, eneo la kaunti ndogo ya Turbo kwenye kaunti ya Uasin-Gishu. Idadi kubwa ya wakazi wa Uasin-Gishu ni Wanandi ambao walihamia eneo hilo kutoka kaunti ya Nandi; kwa hivyo wameingiliana na jamii zingine wa hapa nchini na kimataifa. Sampuli tajwa ilitumiwa kuteua wasailiwa. Nadharia ya ubaada ukoloni iliwaongoza mtafiti kubainisha vipengele vya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi. Hatimaye data iliyokusanywa iliwasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa: Nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kwenye runinga ya Kass zina vipengele vingi vya utamaduni wa jadi katika jamii ya Wanandi. Vilevile, nyimbo hizo zina baadhi ya vipengele vigeni hasa vinavyochangiwa na teknolojia na mwingiliano baina ya Wanandi na jamii zingine. Kadhalika umahuluti wa utamaduni umesaidia nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kutekeleza majukumu yake katika jamii ya sasa. Kwa hivyo, utafiti huu ni muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi na vyombo vya habari hasa kwa wale walimu na wanafunzi watakaotaka kufanya utafiti wa suala la dhima ya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi kwenye jamii za kiafrika.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Identifying and use of imagery in selected songs of Mrisho Mpoto
    (Research Journal in African Languages, 2021-06-18) Mandila, Geoffrey; Opande, Nilson; Simiyu, Fred Wanjala
    Tasnifu hii inalenga kushughulikia nyimbo teule za Mrisho Mpoto. Imeshughulikia jazanda katika nyimbo hizi kwa kutumia nadharia ya kimtindo. Kazi hii inadhamiria kuchanganua jazanda katika nyimbo za Mpoto na jinsi ambavyo jazanda hizo zinachangia kuwasilisha maudhui katika nyimbo hizo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya kimtindo ambayo inahusu matumizi ya maneno kisanaa hivyo basi kuifanya lugha kuwa ngumu au rahisi, kuzua hisia za mwandishi zinaonekana, zikionyesha dhihaka, mapenzi, matumaini, ukali au kejeli, matumizi ya tamathali za usemi kama vile tashbihi, sitiari, tashihisi na kadhalika kwa wingi, uteuzi wa msamiati uliotumika huleta mvuto kwa hadhira lengwa, matumizi ya lugha kwa kujikita katika miktadha maalumu katika kusimulia hadithi au kueleza matukio. Hata hivyo, utafiti huu umejikita katika mihimi mitatu mikuu; maneno hutumiwa kisanaa hivyo basi kuifanya lugha kuwa ngumu au rahisi; hisia za mwandishi zinaonekana, zikionyesha dhihaka, mapenzi, matumaini, ukali au kejeli kutokana na matumizi ya lugha; uteuzi wa msamiati uliotumika huleta mvuto kwa hadhira lengwa. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa nyimbo za Mrisho Mpoto kutokana na matumizi ya jazanda, wapenzi wake wengi hawazielezi vyema. Hivyo basi tukapendekeza tafiti zaidi kufanywa katika nyimbo hizi katika vipengele vingine vya kisanaa.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Kisima Chenye Hekima na Hadithi Nyingine
    (Tunu Publishers, 2026-03-13) Simiyu, Fred Wanjala; Leo, Sanja Leonard
    Mkusanyiko huu ni wa kipekee maanake ni wa kwanza kufanywa na chama cha kitaaluma cha CHAKITA. Hivyo basi, ni kazi ambayo inagusa kina cha roho za wapenzi wote wa lugha hii adhimu ambao ni wanachama. Diwani hii ni ya kwanza katika mchakato mkubwa unaotarajiwa. Kufikia sasa, uandishi wa hadithi fupi umepevuka sana nchini Kenya na kwa wakati huu unashindana na riwaya na labda unapiku uandishi wa tamthilia ambao ni haba. Siyo kwamba tamthilia haziandikwi, la! Zipo tu ingawa hazichapishwi kwa wingi. Muhimu zaidi ni kuhusu toni mbalimbali ambazo tunazishuhudia katika utunzi wa hadithi fupi. Baadhi ya toni hizi ni kero, usisimuzi wa fikra, uchochezi wa hatua mwafaka na hata huzuni. Toni hizi zunatumiwa kuibua masuala mtambuko katika jamii. Pia ikumbukwe kwamba, kipengele hiki cha kimtindo kimechangamkiwa sana na waandishi wa hadithi fupi hivi karibuni.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Maelezo Kinzani ya Vipengele vya Sarufi ya Kiswahili Katika Vitabu Teule vya Shule za Upili Nchini Kenya
    (East African Journal of Swahili Studies, 2021-06-01) Wanyonyi, Fred Wanjala; Misiko, David Wasike; Simiyu, Fred Wanjala
    Dhamira ya makala hii ilikuwa ni kuonesha tofauti za kimaelezo baina ya waandishi wa sarufi kama inavyojitokeza katika ufundishaji na ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili hapa nchini Kenya. Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu na nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba. Sarufi Amilifu ni ya Simon C. Dik (1978). Nadharia hii inashikilia kwamba, uzingatifu wa sarufi ya lugha unadhihirika katika utendaji wa lugha hiyo ambao unakuzwa katika matini inayoandaliwa na wataalamu wake. Nayo nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba iliyoasisiwa na David Allen Kolb mnamo mwaka wa 1984 inaangazia matumizi ya tajiriba katika ufundishaji na ujifunzaji. Kundi lengwa lilikuwa ni waandishi wa Sarufi ya Kiswahili, walimu wa Sarufi ya Kiswahili na wanafunzi wa kidato cha tatu. Tulitumia mbinu za usampulishaji wa kinasibu na usampulishaji wa kimakusudi kuteua sampuli iliyokusudiwa tukizingatia asilimia 30 ya jumla ya idadi lengwa. Walimu 12 na wanafunzi 120 waliteuliwa kushiriki katika uchunguzi huu. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo, hojaji na mahojiano. Data katika makala hii iliwasilishwa kupitia maelezo, majedwali na asilimia. Matokeo ya makala hii yalionesha kwamba, waandishi wa Sarufi ya Kiswahili wanakinzana katika ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vya Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya. Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa walimu wa Sarufi ya Kiswahili, wanafunzi, wataalamu wa Sarufi ya Kiswahili na wale wanaoandaa na kuchapisha vitabu vya Sarufi ya Kiswahili kwa kutambua vipengele tata katika Sarufi ya Kiswahili. Makala ilipendekeza Taasisi ya Ukuzaji wa Mitalaa ya Kenya kuvichunguza upya vitabu vya kiada na ziada vya Sarufi ya Kiswahili ambavyo vimeidhinishwa na wao huku vikiwa na tofauti za kimaelezo.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Masimulizi katika mchakato wa ufundishaji wa kipengele maalum cha msuko katika riwaya ya kidagaa kimemwozea na ile ya chozi la heri
    (Eanso, 2019-08-23) Ndinyo, Stephen Muyundo; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, Deborah
    Masimulizi katika mchakato wa ufundishaji wa vipengele maaalum vya msuko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri. Lengo la Makala haya lilikuwa ni kubainisha namna ambavyo masimulizi yalivyojitokeza katika mchakato wa ufundishaji wa kipengele maalum cha msuko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri. Utafiti huu ulitumia muundo wa kithamano mkabala wa kimfano. Mbinu za ukusanyaji data zilizotumiwa ni uchunzaji usaili na majadiliano ya vikundi viini. Data iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi ,majedwali, nukuu za dondoo kutoka kwa mahojiano. Sampuli lengwa ilihusisha shule 10 kati ya 27, wasailiwa 18 kati ya 54 katika Kaunti ndogo ya Navakholo. Matokeo ni kwamba matukio yalitiririshwa katika mchakato wa ufundishaji wa vipengele maalum vya fani na maudhui katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
    (East African Journal of Swahili Studies, 2020-07-15) Chepkwony, Joyce; Simiyu, Fred Wanjala; Adero, Margan
    Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo. Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo. Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka. Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972. Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga. Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini. Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School. Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70. Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa. Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
    (KIBU, 2020-07-15) Simiyu, Fred Wanjala; Adero, Margan; Chepkwony, Joyce

    Mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini kenya
    (Eanso, 2019-08-23) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, Deborah
    Utafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji na uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu hasa ulilenga kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kudhihirisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundishia uainishaji wa nyimbo darasani na kuonesha namna ambavyo uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki huzisaidia nyimbo husika kutekeleza wajibu wake. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ufundishaji wa fasihi simulizi lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake unakanganya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu inayoonesha utaratibu wa kuainisha fasihi katika misingi ya aina mbalimbali kwa kuegemea miundo na maumbo, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii ambayo inashikilia kuwa ujifunzaji ni mchakato wa utambuzi ambao hujitokeza katika muktadha wa kijamii. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya. Kauli mbiu yake ilikuwa kuboresha umoja wa kitaifa kwa kuunganisha na kuleta watu pamoja. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu na ya kimakusudi. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano na picha. Mtafiti alipata kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulibaini kuwa, tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi darasani. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wana
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya
    (Easo, 2019-08-23) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, Deborah
    Utafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji na uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu hasa ulilenga kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kudhihirisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundishia uainishaji wa nyimbo darasani na kuonesha namna ambavyo uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki huzisaidia nyimbo husika kutekeleza wajibu wake. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ufundishaji wa fasihi simulizi lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake unakanganya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu inayoonesha utaratibu wa kuainisha fasihi katika misingi ya aina mbalimbali kwa kuegemea miundo na maumbo, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii ambayo inashikilia kuwa ujifunzaji ni mchakato wa utambuzi ambao hujitokeza katika muktadha wa kijamii. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya. Kauli mbiu yake ilikuwa kuboresha umoja wa kitaifa kwa kuunganisha na kuleta watu pamoja. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu na ya kimakusudi. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano na picha. Mtafiti alipata kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulibaini kuwa, tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi darasani. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wanafunzi na walimu katika ufundishaji wa nyimbo kama kipera cha fasihi simulizi.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Mwenge Wa Hadithi Fupi: Msingi na Nadharia
    (Tunu Publishers, 2026-03-13) Simiyu, Fred Wanjala; Mohochi, Ernest Sangai; Sanja, Leo Leonard
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu
    (KIBU, 2020-12-01) Simiyu, Fred Wanjala; Wekesa, Winnie Musailo; Opande, Nilson Isaac
    Utafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu
    (Editon Consortium Journal of Kiswahili, 2020-12-10) Wekesa, Winnie Musailo; Simiyu, Fred Wanjala; Opande, Nilson Isaac
    Utafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Remedies on Emerging Lifestyle Diseases
    (KIBU, 2019-06-12) Wekesa, Winnie Musailo; Simiyu, Fred Wanjala
    This paper sets out to explore how universal health care can enhance food security to sustain the development of a society. It focuses on the preventive health care and emerging lifestyle diseases. Lifestyle diseases are those ailments that are linked with the way people live their life; physical and nutritive aspects. They are caused majorly by alcoholism, drug abuse, smoking, lack of physical activities and unhealthy eating habits. The objective of this paper is to explore how food security can be used as a preventive measure to emerging lifestyle diseases. Universal health care are ideals that relate to social and economic progress. Universal health care can mean different things in different contexts. The minimum of it being that no individual or family should suffer financial hardship while accessing quality medical services. This will be achieved by sampling relevant literature written on food security, health care and lifestyle diseases. Food security can serve as a vital means of improving the health and welfare of citizens and lay the foundation for economic growth. A healthy population translates into a productive and stable nation. Therefore, food security exists when all the people at all times have access to sufficient, safe and nutritive foods that meet their dietary needs and food preferences for an active and healthy life.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    The Role of Language in Facilitating Culture: A Case Study of the Isukha Community, Kakamega County in Kenya
    (KIBU, 2019-09-06) Simiyu, Fred Wanjala; Kibigo, Mary Lukamika; Choge, Susan Chebet
    The study explores the role of language specifically nouns in portraying masculinity in the Isukha culture during the ritual of Shilembe and the indigenous sport of Mayo. Culture is the way of life of a people. A people’s culture is encompassed in their language. Thus, it is not possible to delink the Isukha language from their culture especially through the praise poetry that is chanted by the artists during bullfighting. The Isukha community from Shinyalu Sub County of Kakamega County, Kenya, participates in bullfighting as a ritual known as Shilembe. This ritual involves two bulls fighting on the grave of a male hero who has died but while alive he killed either a wild animal or an enemy of the community. They also participate in bullfighting as an indigenous sport that is referred to as Mayo. However, the study discovered that the two games are not just done as a ritual and an indigenous sport respectively during bullfighting but rather the praise poems that are chanted possess language aspects that portray masculinity. The study used Hegemonic Masculinity and Critical Discourse Analysis to analyse the language used by the artists in the praise poems. The findings of this study will be helpful in understanding African communities like the Isukha, especially when it comes to male chauvinism.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Taaluma: Jarida la Chakita
    (Utafiti Foundation, 2026-02-27) Simiyu, Fred Wanjala; Miruka, Fridah
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Tamathali za semi zinazosawiri ubabedume katika majigambo ya miviga ya shilembe na mchezasili wa mayo ya waisukha, nchini kenya kwa mtazamo wa semantiki
    (East African nature & science organization, 2019-09-06) Lukamika, Mary Kibigo; Choge, Susan Chebet; Simiyu, Fred Wanjala
    Makala hii imewasilisha baadhi ya matokeo ya utafiti wa Uzamifu uliotafitia ubabedume katika majigambo ya miviga ya Shilembe na mchezasili wa Mayo katika jamii ya Waisukha nchini Kenya kwa mtazamo wa semantiki. Utafiti huu ulihakiki tamathali mbalimbali za semi ambazo ni chuku, jazanda na majazi miongoni mwa nyingine kwa kutumia mtazamo wa kisemantiki ili kudhihirisha namna zinavyosawiri ubabedume katika miviga ya Shilembe na Mchezasili wa Mayo. Utafiti huu ulifanyika katika Kaunti Ndogo ya Shinyalu, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ya kwanza ni nadharia ya Uwezo-Uume iliyoasisiwa na Robert Bly na kuendelezwa na Izugbara. Inahusu mahusiano ya wanaume na wanawake katika jamii. Nadharia ya pili iliyotumiwa ni ile ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi (UCHAMAWADI). Nadharia hii ina misingi yake katika kazi mbalimbali za wataalam tofauti ulimwenguni. Nadharia mbili zilitumiwa ili kuoanisha taaluma ya Fasihi na Isimu. Utafiti huu ulitumia majigambo kumi na sita kwa kutumia uchunzaji-shiriki, dodoso, unasaji sauti na ujazaji wa hojaji. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa lugha ya majigambo inayoghaniwa na fanani hubeba tamathali za semi zinazosawiri ubabedume. Hivyo, sherehe hizi zitumiwe kama jukwaa la kuelimisha vizazi vichanga vya jamii hii kuhusu mila na desturi zao. Utafiti huu umeonyesha kuwa Fasihi Simulizi ya Mwafrika ni hai. Utafiti umegundua kuwa, lugha ni kipengele muhimu katika jamii. Hata hivyo, utafiti umetambua kuwa, wakati mwingine lugha hutumiwa vibaya na wanajamii kumtukuza Mwanamume kupita kiasi na kumpa uwezo na mamlaka dhidi ya mwanamke. Isitoshe, ubabedume umejengwa katika mila, itikadi na utamaduni wa jamii husika. Makala hii imeweka wazi baadhi ya matokeo ya utafiti huu.
  • «
  • 1 (current)
  • 2
  • »

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback