Browsing by Author "Malugu, Alfred"
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item Athari za Dhana Potofu Kuhusu Afrika na Mwafrika Kwa Jamii ya Waafrika Kama Zinavyodhihirishwa Katika Riwaya Teule za Euphrase Kezilahab(CHAKITA, 2021-11-26) Malugu, Alfred; Mohochi, Ernest Sangai; Mulokozi, Mugyabuso MlinziSuala la dhana potofu kuhusu Afrika na Mwafrika lina historia ndefu sana. Historia yake inaweza kutazamwa kuanzia kipindi cha ukoloni. Dhana hizo potofu kuhusu Afrika na Mwafrika zilijengewa msingi wake sio tu katika vitabu vya dini kama vile Biblia Takatifu, bali pia kwa wanafalsafa na wasomi maarufu wa kale wa Kimagharibi kama vile Carl Meinhof na Georg Hegel. Dhana potofu zilizopandikizwa zilichochea kutawaliwa kwa Waafrika na Afrika kwa jumla. Kwa mfano, kwa kupitia Biblia Takatifu kuna hoja kuwa masaibu, shida, majanga na mambo mbalimbali yanayomsibu Mwafrika yanatokana na kulaaniwa. Kutokana na kuwapo kwa dhana potofu, makala hii inakusudia kutathmini mikakati mbalimbali inayopendekezwa na Euphrase Kezilahabi katika kukabiliana na dhana hizo. Mikakati hiyo itabainishwa kupitia riwaya za Kezilahabi za Gamba la Nyoka, Nagona na Mzingile. Aidha, katika kubainisha dhana hizo, tutaongozwa na baadhi ya mihimili ya Nadharia ya Ubaadaukoloni. Hii ni Nadharia inayofungamanishwa na Edward Said hususani baada ya kuandika kitabu chake cha Orientalism (1978).Item Dhana Potofu Zilizopandikizwa na Wageni Kuhusu Afrika na Mwafrika:(CHALUFAKITA, 2022-03-09) Malugu, Alfred; Mohochi, Ernest Sangai; Mulokozi, Mugyabuso MlinziKwa muda mrefu kumekuwapo na dhana potofu kuhusu Afrika na Mwafrika. Kihistoria, suala hili linaweza kutazamwa kuanzia kipindi cha ukoloni. Msingi mkuu wa dhana hizi potofu kuhusu Afrika na Mwafrika ulijengewa msingi wake katika vitabu vya dini kama vile Biblia Takatifu, na pia mawazo ya wanafalsafa na wasomi maarufu wa kale wa Kimagharibi kama vile Carl Meinhof na Georg Hegel. Dhana potofu zilizopandikizwa zilichochea kutawaliwa kwa Waafrika na Afrika kwa jumla. Kutokana na kuwapo kwa dhana hizo, makala hii inakusudia kubainisha dhana potofu mbalimbali kuhusu Afrika na Mwafrika katika riwaya za Kezilahabi za Gamba la Nyoka, Nagona na Mzingile. Data kwa ajili ya makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini. Mbinu hii ilihusisha utoaji wa maelezo ya kina kuhusu dhana potofu mbalimbali kuhusu Afrika na Mwafrika. Aidha, katika kubainisha dhana hizo, tuliongozwa na baadhi ya mihimili ya Nadharia ya Ubaadaukoloni, ambapo miongoni mwa dhana potofu zilizopandikizwa zilijidhihirisha kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
