Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Kipchirchir, Melly"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 1 of 1
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Mchango wa Kinandi katika Kuihamasisha Jamii kuhusu Ustawi wa Kilimo Kupitia Vipindi vya Runinga ya KASS
    (Jarida la Kiswahili Sanifu, 2025-08-29) Kipchirchir, Melly; Mohochi, Ernest Sangai; Wamalwa, Eric
    Moja kati ya ajenda kuu za serikali ya sasa ya Kenya ni ustawi wa kilimo ambao huleta utoshelevu wa chakula na hivyo kuchangia katika kupunguza gharama ya maisha. Wakulima wengi nchini humo hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Wakati uo huo vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananchi kuhusu kilimo. Lugha ya Kinandi ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass, ni mojawapo ya lugha za kiasili nchini Kenya. Utafiti huu ulilenga kuchunguza mchango wa lugha ya Kinandi katika kuihamasisha jamii kuhusu ustawi wa kilimo kupitia vipindi vya kilimo katika runinga ya Kass. Utafiti ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano ya Hymes (1972). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Isitoshe watangazaji 9 vilevile walihusishwa. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu jinsi wanajamii huhamasishwa kuhusu ustawi wa kilimo kupitia vipindi vya kilimo katika runinga ya KASS.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback