Matumizi ya tarakilishi katika ufundishaji wa fasihi simulizi katika shule za upili nchini Kenya: Uchunguzi kifani wa kaunti ya Bungoma
dc.contributor.author | Kibiti, David Barasa | |
dc.date.accessioned | 2019-03-19T15:04:23Z | |
dc.date.available | 2019-03-19T15:04:23Z | |
dc.date.issued | 2018-05 | |
dc.description | Matumizi ya Tarakilishi Katika Ufundishaji wa Fasihi Simulizi Katika Shule za Upili Nchini Kenya: Uchunguzi Kifani wa Kaunti ya Bungoma | en_US |
dc.description.abstract | Matumizi ya teknolojia za kisasa katika mawasiliano ni muhimu sana leo. Katika muktadha wa elimu, mbinu za kurahisisha mawasiliano darasani ni muhimu ili kuhakikisha matokeo mema katika mtihani na pia kuwaandaa wanafunzi katika matumizi ya vifaa vya kisasa wanapomaliza shule. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu matumizi ya tarakilishi katika shughuli za elimu lakini hapana wowote tulioshuhudia unaohusu ufunzaji wa Fasihi Simulizi kwa kutumia tarakilishi. Pengo hili ndilo ambalo limejenga msingi wa utafiti huu. Basi katika utafiti huu, Mtafiti alichunguza matumizi ya tarakilishi katika ufunzaji wa Fasihi Simulizi. Utafiti huu hasa ulilenga kutathmini ni kwa kiwango kipi walimu wa Kiswahili hutumia tarakilishi katika kufunza Fasihi Simulizi. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Ukubalifu na Utumizi wa Teknolojia iliyoasisiwa na Rogers (2003). Nadharia hii inafafanua hatua wanazopitia watumizi kabla ya kuanza kutumia teknolojia mpya katika shughuli zao. Utafiti uliegemea muundo wa kithamano na mkabala wa usoroveya na ulifanywa katika shule teule za upili katika kaunti ya Bungoma. Sampuli ya shule 18 iliteuliwa katika jumla ya shule teule za kaunti ndogo katika kaunti nzima. Shule hizi zimepandishwa vyeo mwaka wa 2010 na kufanywa kuwa shule teule katika kila eneo bunge. Wasailiwa walipatikana kutoka kwa jumla ya shule 314 za kaunti ya Bungoma. Sampuli ilijumlisha walimu wa Kiswahili 36, walimu wakuu 18 wa shule zilizoteuliwa. Jumla ya watafiti walikuwa 54. Mbinu za kuteua sampuli zilikuwa sampuli maksudi, sampuli nasibu tabakishi na sampuli nasibu. Utafiti huu ulitumia hojaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Hatimaye, data hizo zikawasilishwa na kuchanganuliwa kwa majedwali, nambari na asilimia. Mtafiti alipata kwamba shule zote kati ya zilizoteuliwa zina tarakilishi. Hata hivyo, hizi tarakilishi hazikutumiwa na walimu katika shughuli za kufunza darasani. Pia, ilibainika kuwa kuna changamoto zinazoathiri matumizi ya tarakilishi kama wenzo wa kufunzia. Mfano mwema ni ukosefu wa ujuzi wa tarakilishi miongoni mwa walimu na umeme usiotegemewa. Inatarajiwa kwamba matokeo yatawasaidia walimu kuboresha mbinu za ufunzaji hasa wa Fasihi Simulizi kwa kutumia teknolojia za kisasa. Serikali na wadau katika elimu watayaboresha mazingira ya elimu. | en_US |
dc.identifier.uri | http://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/251 | |
dc.language.iso | Swahili | en_US |
dc.publisher | Kibabii University | en_US |
dc.rights | Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States | * |
dc.rights.uri | http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/ | * |
dc.subject | Kiswahili | en_US |
dc.title | Matumizi ya tarakilishi katika ufundishaji wa fasihi simulizi katika shule za upili nchini Kenya: Uchunguzi kifani wa kaunti ya Bungoma | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |