Tathmini ya vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Busia
dc.contributor.author | Abai, Rose Ajuma | |
dc.date.accessioned | 2019-03-20T09:25:17Z | |
dc.date.available | 2019-03-20T09:25:17Z | |
dc.date.issued | 2018-04 | |
dc.description.abstract | Vitabu vya kiada ni nyenzo kuu hasa katika mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji. Ni vigumu kuafikia malengo ya elimu bila vitabu vya kiada. Ni muhimu kuteua kitabu cha kiada kinachofaa.Ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili kama msingi wa kukuza lugha ni jambo gumu linalohitaji kutiliwa maanani. Utafiti huu ulipata msukumo kutokana na hali kwamba vitabu mbalimbali vya kiada vimeidhinishwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala Nchini Kenya kwa mitindo tofauti tofauti, kwa utaratibu wa sasa wa biashara huria ya vitabu na ubinafsishaji. Somo moja huweza kuwa na vitabu kadhaa. Ni kwa misingi hiyo ndipo utafiti huu ulidhamiria kutathmini vitabu vitatu vya kiada katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili kwa shule za msingi katika kaunti dogo ya Teso Kaskazini Kaunti ya Busia. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha athari za matumizi ya vitabu vya kiada aina aina katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili, kisha kuchanganua mitazamo tofauti ya waandishi katika kueleza vipengele vya sarufi na kupambanua Nguvu Udhaifu Nafasi na Tishio (NGUNATI) ya vitabu vya kiada vya wanafunzi katika ufundishaji wa sarufi ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Masharti ya Ujifunzaji. Nadharia hii inasisitiza kushirikishwa kwa michakato ndani ya akili ya binadamu katika kufanikisha ujifunzaji. Muundo wa kimaelezo na kitakwimu na mkabala wa usoroveya ulitumiwa. Umma lengwa ya utafiti huu ilikuwa shule ishirini na nane (28) za msingi zilizoteuliwa kutumia mbinu ya kishada kutoka kwa jumla ya shule themanini na saba (87) zinazopatikana katika kaunti dogo la Teso Kaskazini. Jumla ya walimu ishirini na nane (28) wa somo la Kiswahili waliteuliwa kutumia mbinu ya kimaksudi na wanafunzi mia tatu arobaini na nne (344) waliteuliwa kutumia mbinu ya kinasibu. Jumla ya wasailiwa walikuwa 372. Data katika utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji na uchanganuzi wa yaliyomo katika vitabu vitatu vya kiada vya Kiswahili. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia majedwali na asilimia. Data iliwasilishwa kwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano. Utafiti umebainisha kuwa walimu hutumia kitabu kimoja cha kiada. Kimsingi matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa, kuna haja ya kutathmini na kufanya marekebisho katika vitabu vya kiada vinavyotumika katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ili mahitaji ya wanafunzi yaweze kuafikiwa. Utafiti huu una mchango katika kuelewa uhalisia kuhusu vitabu vya kiada vinavyotumiwa katika shule nchini Kenya. Aidha, matokeo haya yanatarajiwa kuwapa washika dau mfumo wa kinadharia katika kutathmini vitabu vya kiada vinavyofaa kutumiwa katika ufundishaji wa sarufi ya Kiswahili. | en_US |
dc.identifier.uri | www.kibu.ac.ke | |
dc.identifier.uri | http://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/259 | |
dc.language.iso | Swahili | en_US |
dc.publisher | KIBU | en_US |
dc.rights | Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States | * |
dc.rights.uri | http://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/ | * |
dc.title | Tathmini ya vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Busia | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Abai-Tathmini ya vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Busia.pdf
- Size:
- 117.15 KB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: