Changamoto zinazowakumba vijana katika tamthilia ya Kitumbua kimeingia mchanga

dc.contributor.authorMwangi, Jackson Ndung’u
dc.date.accessioned2019-03-29T07:10:32Z
dc.date.available2019-03-29T07:10:32Z
dc.date.issued2018-06-12
dc.description.abstractKatika ulimwengu wa sasa, kuna mabadiliko chungu nzima yanayoshuhudiwa duniani kote yanasababishwa na masuala anuwai kama vile maendeleo ya kiteknolojia pamoja na utandarithi yanayoathiri pakubwa maisha ya vijana. Hapo nchini, vijana wana umuhimu wa kipekee kwani wanatekeleza majukumu muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi. Isitoshe, idadi ya vijana kote ulimwenguni imeendelea kuongezeka kila uchao na imepiku ile ya wazee. Kwa hivyo, ni nyema kujadili changamoto zinazowakabili na kupendekeza hatua za kukabiliana nazo. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchanganua changamoto zinazowakumba vijanapamojanaathari zake katika ya tamthilia ya Kitumbua Kimeingia MchangayaS.A Mohamed (2000).Mada hiiilichaguliwakwamisingikwambavijanawanakumbwanachangamoto nyingikatikamaishayao zinazowaathiri kwa kiasi cha haja na kutinga juhudi za kuafikia jaala zao.Utafiti huu ulilenga kubainisha changamoto zinazowakumba vijanakatika tamthilia hii na kutambua mbinu ambazo vijana hawa wanazua ili kukabiliana nazo. NadhariayaUhalisiailitumika kwa sababuilionekana kufaa zaidi kuchanganua changamoto zinazowakumba vijana kwani changamoto hizi zina uhalisiamkubwakatikamaishayao. Madhumuniyautafiti huu yalikuwa ni kuchunguzanakueleza namna changamoto za vijana zinavyojitokeza katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga na kisha kubainisha hatua zinazochukuliwa kuzitatua changamoto hizo. Utafiti huu ni wa kimaelezo na kiudhamano kwani ulihusisha kuchanganua matini zinazohusiana na mada husika. Sampuli katika utafiti huu iliteuliwa kimakusudi kwani ndiyo ingempa mtafiti data aliyonuia kuipata. Utafiti huu ulijikita katika maktaba ya kitaifa na yale ya vyuo vikuu humu nchini. Utafitiwetuumebainisha kidakidaki kwambatamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga imesheheniChangamoto nyingi mno zinazowaathiri vijana kamavile dawa za kulevya, dhuluma,anasa,uavyaji mimba,utabaka, athari za tamadunizakigenipamoja nakufanyiwa uamuzi.Aidha, imethihirika wazikuwa vijana wanazua mbinu kabambe za kutatua changamoto zinazowakumba kama vile kutafuta ushauri kutoka kwa wenzao, kutumia wazee na kuwa na ujasiri wa kujitetea dhidi ya wanaowadhulumu pamoja na serikali kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya. Ni bayana kuwa utafiti huu utaifaa jamii ya wasomi wanaoshughulikia maswala ibuka katika jamii. Inapendekezwa kuwa tafiti za baadaye zitafiti kuhusu nafasi ya vijana katika jamii.en_US
dc.identifier.isbn978-9966-59-011-5
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/443
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKIBUen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.subjectDhana ya Vijanaen_US
dc.subjectJaalaen_US
dc.subjectChangamotoen_US
dc.subjectAtharien_US
dc.subjectUhalisiaen_US
dc.titleChangamoto zinazowakumba vijana katika tamthilia ya Kitumbua kimeingia mchangaen_US
dc.typeWorking Paperen_US

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mwangi Jackson Ndung’u.pdf
Size:
52 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections