Browsing by Author "Simiyu, Fred, C. N. W."
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item The Hybrid Aesthetics of the Underdog: A Postcolonial Reading of Wadagliz’s Viral Song, Anguka Nayo(Journal of Linguistics, Literary and Communication Studies, 2026-03-17) Simiyu, Fred, C. N. W.This paper seeks to characterise Gengetone popular music as a site for understanding the nature and function of postcolonial cultural productions. The study is largely inspired by Homi Bhabha’s proposition that the present is often a meeting place of the past and the present. A place of constantly changing, as opposed to perpetual, identities; a fluid space of what was and what is ensuing. The study is therefore founded on the premise that just like its unstable context, Gen-Z music—often coming through as non-conformism—may best represent the artistic value of popular art in an increasingly modernising context that is intensely shaped by the mass culture. The song that forms the basis of the present study, Anguka Nayo, was purposively sampled and subjected to close reading through the lenses of Homi Bhabha’s theory of hybridity. The main finding of the study is that, just like most other contemporary cultural artefacts, popular music can indeed provide interesting insights into the hybrid nature of contemporary cultural artefacts. The study, therefore, adds to existing perspectives on postcolonial discourses, especially hybridity.Item Uasi au Utatu katika Ujitambulishaji wa Wanajenizi: Matumizi ya Mihadarati katika Nyimbo za Gengetone(Journal of Kiswahili and Other African Languages, 2026-03-17) Simiyu, Fred, C. N. W.Makala hii inahusu matumizi ya uasi ndani ya utatu kama mkakati wa kutambulisha vijana wa Jenizi kupitia nyimbo za Gengetone. Fasihi simulizi kupitia kipera kimojawapo cha nyimbo za gengetone, inatumiwa kupinga na au kuhimiza matumizi ya mihadarati kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali. Kwa jicho la haraka, inaonekana kuwa, baadhi ya waimbaji wa gengetone wanashabikiwa ukiukaji wa ukawaida wa kijami. Hata hvivo, kwa kutumia jicho la ndani, imebainika kuwa, wasanii hawa wanapinga mifumo dhalimu ya kijamii na kupendekeza mwamko mpya. Kwa hivyo, ni muhimu kuchanganua nyimbo teule za gengetone kwa jicho la ndani ili kubainisha kiini chake. Kutokana na haya, makala hii inachunguza mikakati inayotumiwa kuasi ukawaida, matumizi ya uasi kama silka ya ujitambulishaji; na matumizi ya utatu kama mkakati wa kupinga unyanyaswaji wa wanyonge kupitia nyimbo za gengetone. Haya yamebainishwa katika makala haya, ambapo uchambuzi wa nyimbo tano za gengetone umefanywa kwa kuongozwa na Nadharia ya Utatu. Uchambuzi wa data katika makala hii umedhihirisha kwamba nyimbo za Gengetone zinakua kwa kasi kikubwa sana kutokana na uwezo wake wa kujinyambua, ili kupanua mipaka yake. Ujinyambuaji huu unafanywa kwa kuchopeka mitindo mipya ili kuendelea kuwa hai, kuvutia na kusisimua. Isitoshe, Gengetone siyo tu aina ya muziki, bali ni aina maalum ya ujitambulishaji wa vijana wa mjini. Huu ni mfano mzuri wa nguvu za sanaa zinazotumiwa kuvunja kuta za ukabila, kuunganisha tamaduni mbalimbali, na kutoa jukwaa la kuwawezesha vijana kutoa sauti zao. Ni jukwaa la utatu ambalo linaloonesha ukakamavu, ubunifu na uzalendo wa vijana wa mjini.
