Browsing by Author "Opande, Nilson"
Now showing 1 - 1 of 1
- Results Per Page
- Sort Options
Item Identifying and use of imagery in selected songs of Mrisho Mpoto(Research Journal in African Languages, 2021-06-18) Mandila, Geoffrey; Opande, Nilson; Simiyu, Fred WanjalaTasnifu hii inalenga kushughulikia nyimbo teule za Mrisho Mpoto. Imeshughulikia jazanda katika nyimbo hizi kwa kutumia nadharia ya kimtindo. Kazi hii inadhamiria kuchanganua jazanda katika nyimbo za Mpoto na jinsi ambavyo jazanda hizo zinachangia kuwasilisha maudhui katika nyimbo hizo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya kimtindo ambayo inahusu matumizi ya maneno kisanaa hivyo basi kuifanya lugha kuwa ngumu au rahisi, kuzua hisia za mwandishi zinaonekana, zikionyesha dhihaka, mapenzi, matumaini, ukali au kejeli, matumizi ya tamathali za usemi kama vile tashbihi, sitiari, tashihisi na kadhalika kwa wingi, uteuzi wa msamiati uliotumika huleta mvuto kwa hadhira lengwa, matumizi ya lugha kwa kujikita katika miktadha maalumu katika kusimulia hadithi au kueleza matukio. Hata hivyo, utafiti huu umejikita katika mihimi mitatu mikuu; maneno hutumiwa kisanaa hivyo basi kuifanya lugha kuwa ngumu au rahisi; hisia za mwandishi zinaonekana, zikionyesha dhihaka, mapenzi, matumaini, ukali au kejeli kutokana na matumizi ya lugha; uteuzi wa msamiati uliotumika huleta mvuto kwa hadhira lengwa. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa nyimbo za Mrisho Mpoto kutokana na matumizi ya jazanda, wapenzi wake wengi hawazielezi vyema. Hivyo basi tukapendekeza tafiti zaidi kufanywa katika nyimbo hizi katika vipengele vingine vya kisanaa.
