Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Ngugi, Pamela Muhadia Yalwala"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 1 of 1
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika Upya wa Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’
    (East African Journal of Swahili Studies, 2024-07-11) Kinara, Gladys; Ngugi, Pamela Muhadia Yalwala; Wafula, Richard Makhanu
    Makala hii inalenga kuchunguza mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika upya wa tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi waAdili’ Robert (1967). Mapokeo yanaweza kuelezwa kama mila, desturi, fikra na hisia za kihistoria zinazohusu mtazamo sio tu wa yaliyopita zamani lakini pia uwepo wa mambo ya kihistoria na ya sasa kwa lengo la kuyapitisha kwa jamii (Sangi na wengine, 2012). Uchambuzi wa kazi hii umeegemezwa katika mihimili ya nadharia ya Bakhtin (1981) inayoshikilia kwamba lugha huwa na nguvu za Kani Kitovu na Kani Pewa. Kiwango cha Kani Kitovu huhusu nguvu za kisheria zinazotambulisha lugha. Hizi ni sheria za kisarufi na hazibadiliki. Katika muktadha wa fasihi, nguvu hizi zinawakilisha utamaduni wa jamii ambao daima unabaki kurithishwa na kufuatwa kama kanuni. Kiwango cha Kani Pewa nacho kinatokana na matumizi ya lugha katika jamii yanayobadilika kiwakati na yanatofautisha taaluma, tabaka na matumizi mengine ya lugha katika jamii. Nguvu za Kani Pewa zinajaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi. Katika kiwango cha fasihi, nguvu za Kani Kitovu zinawakilisha utamaduni wa jamii ambao daima unabaki kurithishwa na kufuatwa kama kanuni. Kwa upande mwingine, kiwango cha Kani Pewa kinatokana na matumizi ya lugha katika jamii yanayobadilika kiwakati na yanayotofautisha taaluma, tabaka na matumizi mengine ya lugha katika jamii. Nguvu za Kani Pewa zinajaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi. Katika kiwango cha fasihi, nguvu za Kani Pewa zinawakilisha upya na katika muktadha huu Utenzi wa Mwana Kupona katika tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’. Utafiti ulikuwa wa kimaelezo na ulifanywa maktabani na nyanjani. Sampuli ya maktabani na nyanjani iliteuliwa kimakusudi. Maktabani, mtafiti alisoma kwa kina matini iliyochapishwa kwa lengo la kupata data ya msingi. Nyanjani, mtafiti alifanya mahojiano na majadiliano na wanajamii walioteuliwa katika kukusanya data. Data kutoka katika tenzi zilizoteuliwa, maandishi yaliyohusu utafiti, data ya nyanjani zilichambuliwa kulingana na lengo la makala haya na mihimili ya nadharia kwa lengo la kuonyesha namna mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona yalivyobainika katika upya wa maandishi ya tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na’ Utenzi wa Adili’. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kwamba Shaaban Robert (1967) katika kuandika ‘Utenzi wa Hati’ na’ Utenzi wa Adili’ aliazima pakubwa kutoka katika Utenzi wa Mwana Kupona mbali na kuongeza upya kwa mujibu wa hali ya kijamii ya wakati wake.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback