Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Misiko, David Wasike"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 3 of 3
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Lugha kama rasilimali ya jamii: uchunguzi wa redio za fm zinazotumia kibukusu katika kaunti ya bungoma
    (Moi University, 2017-01-12) Misiko, David Wasike
    Matumizi ya lugha za kiasili yameshutumiwa na watu wengi kwa kukuza ukabila haswa nchini Kenya. Hata hivyo, lugha hizi zinaweza kuwa rasilimali kwa wazungumzaji zikitumiwa vyema. Utafiti huu ulilenga kuchunguza lugha za kiasili zinavyojitokeza kama rasilimali kwa wazungumzaji wake zinapotumika katika redio za FM. Aidha, utafiti ulinuia kujadili jinsi matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yanavyowezesha jamii husika kupata habari zinazoziwezesha kuboresha hali zao za maisha kwa njia mbalimbali. Uchunguzi ulidhamiria hususan: Kuhakiki yaliyomo katika vipindi vya jamii, uchumi, siasa na afya vinavyowasilishwa kwa kutumia Kibukusu katika redio za FM, zinazosikika katika kaunti ya Bungoma; Kutathmini Kibukusu kinavyojitokeza kama rasilimali kuangazia masuala ya jamii, uchumi, siasa na afya kwa wazungumzaji wake kinapotumika katika redio za FM, kisha kutambua changamoto za matumizi ya Kibukusu kama rasilimali kwa wakaazi wa Bungoma kupitia vituo vya redio za FM. Utafiti ulitumia mbinu za ustahilivu na kikiasi. Lahaja ya Kibukusu ilitafitiwa katika mazingira halisi ambapo lugha hiyo hutumika na wazungumzaji wake. Miktadha ya matumizi ya Kibukusu ilichunguzwa, hususan kama rasilimali kwa wazungumzaji wake. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili; Sarufi Amilifu ya Halliday na ya Uanzilishi wa Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Show. Sarufi Amilifu ilihusishwa katika uchanganuzi wa vipindi vinavyopeperushwa kwa kutumia lugha za kiasili. Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa vipindi vinavyopeperushwa na vituo hivyo viwili vya redio. Uchunguzi ulifanywa katika vituo vya Sulwe na West FM vinavyopeperusha matangazo kwa Kibukusu katika kaunti ya Bungoma. Utafiti ulihusisha mhariri mmoja, watangazaji wawili na wataalamu wanne; mmoja kwa kila mojawapo ya masuala haya; jamii, uchumi, afya na siasa ambao hualikwa kwa kila mojawapo ya vituo hivyo. Vilevile, wasikilizaji 70 kutoka kila mojawapo ya vituo hivyo viwili vya redio walihusishwa. Kwa jumla, utafiti uliwahusisha watu 154. Wasikilizaji hao waliteuliwa kutoka kwa kaunti ndogo sita za kaunti ya Bungoma na walihusisha jinsia zote. Wasikilizaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimakusudi ambao huwezesha idadi ya wahojiwa kuongezeka kadiri utafiti unavyoendelea. Vipindi vya redio vya vituo vyote viwili vilivyohusiana na masuala ya jamii, afya, uchumi na siasa vilisikilizwa. Mbinu ya ujazaji wa hojaji kwa watangazaji na wasikilizaji, usaili wa wahariri, watangazaji na wataalamu na kurekodi vipindi mahususi zilitumika. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa wanahabari, hohaji kwa wasikilizaji, mwongozo wa usaili kwa wahariri, watangazaji na wataalamu na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sarufi Amilifu. Data ifuatayo ilikusanywa: vipindi vya redio vinavyotumia lahaja ya Kibukusu, yaliyomo katika vipindi hivyo, Kibukusu kinavyojitokeza kama rasilimali kwa wazungumzaji wake na changamoto za matumizi ya lahaja hiyo katika redio za FM. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kwa maelezo na takwimu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa yafuatayo: Matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yalijaza pengo liliokuwepo katika upashaji habari kwa watu walioko mashinani; Matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yaliwezesha wazungumzaji kufikia maamuzi faafu kuhusiana na masuala ya afya, siasa, uchumi na jamii; ukosefu wa taasisi ya kudhibiti uundaji wa istilahi ni mojawapo ya changamoto zinazokumba matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM. Matokeo ya utafiti huu yalitoa picha halisi ya mchango wa lugha za kiasili katika redio za FM nchini Kenya kwa maendeleo ya jamii husika. Matokeo ya uchunguzi huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu matumizi ya lugha za Kiafrika katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utawafaidi wapangaji lugha kitaifa na katika viwango vya kaunti. Utafiti huu pia unatarajiwa kutoa mchango kwa uhifadhi na makuzi ya lugha za Kiafrika kichanya. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Kuundwa kwa taasisi za kutafiti, kuunda na kudhibiti istilahi zinazotumika katika lugha za kiasili; Vyuo vikuu kufundisha baadhi ya lugha hizi za kiasili ili kubadilisha mtazamo hasi kuzihusu; Serikali za kaunti kuanzisha sera za lugha katika viwango vya kaunti na hatimaye, kufufuliwa kwa ufundishaji wa lugha za kiasili mbali na Kiingereza, Kiswahili na lugha zingine za kigeni kama vile Kifaransa na Kijerumani katika sera ya lugha nchini Kenya.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Maelezo Kinzani ya Vipengele vya Sarufi ya Kiswahili Katika Vitabu Teule vya Shule za Upili Nchini Kenya
    (East African Journal of Swahili Studies, 2021-06-01) Wanyonyi, Fred Wanjala; Misiko, David Wasike; Simiyu, Fred Wanjala
    Dhamira ya makala hii ilikuwa ni kuonesha tofauti za kimaelezo baina ya waandishi wa sarufi kama inavyojitokeza katika ufundishaji na ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili hapa nchini Kenya. Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu na nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba. Sarufi Amilifu ni ya Simon C. Dik (1978). Nadharia hii inashikilia kwamba, uzingatifu wa sarufi ya lugha unadhihirika katika utendaji wa lugha hiyo ambao unakuzwa katika matini inayoandaliwa na wataalamu wake. Nayo nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba iliyoasisiwa na David Allen Kolb mnamo mwaka wa 1984 inaangazia matumizi ya tajiriba katika ufundishaji na ujifunzaji. Kundi lengwa lilikuwa ni waandishi wa Sarufi ya Kiswahili, walimu wa Sarufi ya Kiswahili na wanafunzi wa kidato cha tatu. Tulitumia mbinu za usampulishaji wa kinasibu na usampulishaji wa kimakusudi kuteua sampuli iliyokusudiwa tukizingatia asilimia 30 ya jumla ya idadi lengwa. Walimu 12 na wanafunzi 120 waliteuliwa kushiriki katika uchunguzi huu. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo, hojaji na mahojiano. Data katika makala hii iliwasilishwa kupitia maelezo, majedwali na asilimia. Matokeo ya makala hii yalionesha kwamba, waandishi wa Sarufi ya Kiswahili wanakinzana katika ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vya Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya. Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa walimu wa Sarufi ya Kiswahili, wanafunzi, wataalamu wa Sarufi ya Kiswahili na wale wanaoandaa na kuchapisha vitabu vya Sarufi ya Kiswahili kwa kutambua vipengele tata katika Sarufi ya Kiswahili. Makala ilipendekeza Taasisi ya Ukuzaji wa Mitalaa ya Kenya kuvichunguza upya vitabu vya kiada na ziada vya Sarufi ya Kiswahili ambavyo vimeidhinishwa na wao huku vikiwa na tofauti za kimaelezo.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Matumizi ya Maigizo kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenya
    (KIBU, 2019-08-23) Misiko, David Wasike; Simbi, Inviolata Wekesa; Amukowa, Deborah Wanyama; Masinde, Edwin
    Utafiti huu ulilenga kuonyesha matumizi ya maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia; mfano wa Kigogo katika shule za upili, Kaunti ya Bungoma Kusini. Ufundishaji wa somo lolote hujikita kwenye mawasiliano baina ya mwalimu na mwanafunzi. Mbinu za kufundisha huwa viungo muhimu vya kufanikisha mawasiliano haya. Mwalimu ana jukumu la kuteua mbinu mwafaka ya kufundisha. Kuna mbinu mbalimbali mwalimu anaweza kutumia kufundisha tamthilia. Utafiti huu umechagua maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza iwapo walimu wanatumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia na wanatumia kwa jinsi gani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utendaji inayoshikilia kuwa matini ya kidrama huwasilisha ujumbe vyema zaidi kupitia uigizaji wake katika jukwaa. Utafiti ulilenga shule kumi na sita kati ya shule hamsini na mbili. Walimu wanaofundisha Kiswahili kidato cha tatu na nne pamoja na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne ndio waliolengwa. Watafitiwa waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya utabakishaji, kinasibu na usampulishaji kimaksudi. Stadi ya utabakishaji ilitumika kuainisha shule katika makundi matatu. Mbinu ya kimaksudi ilitumika kuteua shule tatu za kaunti na walimu wanaofundisha kiswahili kidato cha tatu na nne. Mbinu ya kinasibu ilitumika kuteua shule za kaunti ndogo, shule kumi na mbili na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Wanafunzi kumi katika kila kidato waliteuliwa, jumla ya wanafunzi mia tatu ishirini walitafitiwa. mbinu zlizotumika kukusanya data zilikuwa hojaji, maswali ya usaili na uchunzaji. Maswali ya usaili yalitumika kukusanya data kutoka kwa walimu. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia maelezo, asilimia, picha na majedwali. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kuwa walimu 83% ndio walitumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia ya Kigogo. Utafiti unapendekeza kuwa mbinu za maigizo ambazo hazitumiki pia zitumike ili kuboresha ufundishaji. Vile vile taasisi ya elimu kuandaa semina na warsha za kuwahamasisha walimu kuhusu njia mbalimbali za kutumia maigizo kufundisha. Aidha kila shule iwe na klabu cha maigizo ili kutumika katika ufundishaji wakati wowote.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback