Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Masinde, Edwin"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 2 of 2
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Matumizi ya Maigizo kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenya
    (KIBU, 2019-08-23) Misiko, David Wasike; Simbi, Inviolata Wekesa; Amukowa, Deborah Wanyama; Masinde, Edwin
    Utafiti huu ulilenga kuonyesha matumizi ya maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia; mfano wa Kigogo katika shule za upili, Kaunti ya Bungoma Kusini. Ufundishaji wa somo lolote hujikita kwenye mawasiliano baina ya mwalimu na mwanafunzi. Mbinu za kufundisha huwa viungo muhimu vya kufanikisha mawasiliano haya. Mwalimu ana jukumu la kuteua mbinu mwafaka ya kufundisha. Kuna mbinu mbalimbali mwalimu anaweza kutumia kufundisha tamthilia. Utafiti huu umechagua maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza iwapo walimu wanatumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia na wanatumia kwa jinsi gani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utendaji inayoshikilia kuwa matini ya kidrama huwasilisha ujumbe vyema zaidi kupitia uigizaji wake katika jukwaa. Utafiti ulilenga shule kumi na sita kati ya shule hamsini na mbili. Walimu wanaofundisha Kiswahili kidato cha tatu na nne pamoja na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne ndio waliolengwa. Watafitiwa waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya utabakishaji, kinasibu na usampulishaji kimaksudi. Stadi ya utabakishaji ilitumika kuainisha shule katika makundi matatu. Mbinu ya kimaksudi ilitumika kuteua shule tatu za kaunti na walimu wanaofundisha kiswahili kidato cha tatu na nne. Mbinu ya kinasibu ilitumika kuteua shule za kaunti ndogo, shule kumi na mbili na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Wanafunzi kumi katika kila kidato waliteuliwa, jumla ya wanafunzi mia tatu ishirini walitafitiwa. mbinu zlizotumika kukusanya data zilikuwa hojaji, maswali ya usaili na uchunzaji. Maswali ya usaili yalitumika kukusanya data kutoka kwa walimu. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia maelezo, asilimia, picha na majedwali. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kuwa walimu 83% ndio walitumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia ya Kigogo. Utafiti unapendekeza kuwa mbinu za maigizo ambazo hazitumiki pia zitumike ili kuboresha ufundishaji. Vile vile taasisi ya elimu kuandaa semina na warsha za kuwahamasisha walimu kuhusu njia mbalimbali za kutumia maigizo kufundisha. Aidha kila shule iwe na klabu cha maigizo ili kutumika katika ufundishaji wakati wowote.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Matumizi ya Riwaya Katika Kutoa Muktadha wa Ufafanuzi wa Muundo wa Sentensi Katika Shule za Upili, Kaunti Ndogo ya Webuye Magharibi
    (East African Journal of Swahili Studies, 2019-07-26) Soita, Elizabeth Nakhumicha; Masinde, Edwin; Wekesa, Ben Nyongesa
    Kwa muda mrefu mafunzo ya lugha na fasihi yamekuwa yakitengwa ingawa silabasi ya K.I.E. (2002) ilipendekeza mwalimu anapofundisha atumie mwelekeo msetokwa sababu silabasi hii iliorodheresha tu mada za fasihi na lugha bila kutoa mwelekeo wa utekelezaji. Hali hii ilimpa mtafiti msukumo wa kufanya utafiti kuhusu matumizi ya riwaya katika kutoa muktadha wa ufafanuzi wa muundo wa sentensi katika shule za upili, kaunti ndogo ya Webuye Magharibi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha matumizi ya riwaya katika kutoa muktadha wa ufafanuzi wa muundo wa sentensi na utekelezaji wake shuleni. Nadharia jumuishi ya ufundishaji wa lugha iliyoasisiwa na Hammerly (1985) ilitumika katika utafiti. Muundo wa usoroveya-elezi ulitumika katika utafiti huu. Shule 17 zilifanyiwa utafiti. Idadi ya walimu 35 na wanafunzi 43 walitafitiwa. Deta ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, mahojiano na utathmini wa maazimio ya kazi, mipangilio ya masomo na mitihani. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa riwaya inaweza kutoa muktadha wa ufafanuzi wa muundo wa sentensi ingawa changamoto ni kuwa asilimia 68.57 ya walimu hawakutambua pendekezo la silabasi ya K.I.E (2002) la ufundishaji wa mwelekeo mseto. Walimu 11 (31.43%) walikuwa na ufahamu wa kuseta. Walimu 7 kwa 11(63.63%) walipata ugumu wa kutekeleza ufundishaji mseto. Walimu 4 kwa 11 (11.43%) walifundishariwaya pamoja na muundo wa sentensi wala si kufundisha muundo wa sentensi kwa kutumia riwaya. Walimu 31 kwa 35 ambao hawakuzingatia mwelekeo mseto katika ufundishaji wa muundo wa sentensi kwa kutumia riwaya walionyesha uwezekano wa riwaya kuweza kutumika kufundisha muundo wa sentensi. Mtafiti alipendekeza walimu wahamasishwe kuhusu utekelezaji wa mwelekeo mseto wa fasihi na lugha darasani ili kuboresha lugha kwa ujumla. Kwa mujibu wa utafiti huu, vitabu vya riwaya vinapaswa kuteuliwa kwa uangalifu ili viwena manufaa kwa ufundishaji wa muundo wa sentensi.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback