Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Magambo, Emilly Angushi"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 3 of 3
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Dhima ya Futuhitandao Katika Kukabiliana na Masuala ya Afya ya Akili Miongoni Mwa Wakenya
    (Eastern Africa Journal of Kiswahili, 2025-06-09) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Orina, Felix Ayioka
    Fasihi kupitia utambuzi na tanzu zake tofauti tofauti, tangu jadi, imekuwa na majukumu mahususi ya kutekeleza katika jamii. Kama utanzu mojawapo wa fasihi simulizi, futuhi imetumika pakubwa katika vyombo vya habari kama vile televisheni na redioni kuwafurahisha na kuwachekesha watazamaji na wasikilizaji. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, futuhi imechukua mkondo tofauti katika uwasilishaji wake. Hii ni kwa sababu ya njia mpya ya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa ambayo imezua mitandao ya kijamii kama vile Facebook, TikTok, Twitter, Instagram na YouTube. Mbinu mpya za kiteknolojia sasa zipo kwa wingi kuliko wakati mwingine wowote. Licha ya mkurupuko wa mbinu hizi, tusisahau kwamba tangu jadi futuhi imekuwa muhimu katika jamii mbalimbali. Lakini sasa futuhi imekuwa karibu zaidi kwa sababu ya teknolojia ya kisasa. Vile vile, suala la afya ya akili limekuwa nyeti miongoni mwa Wakenya. Hivyo basi, kukawa na haja ya kuchunguza zaidi kuhusu futuhi katika mitandao hii ya kijamii na afya ya akili miongoni mwa Wakenya. Mada hii vile vile ilichaguliwa kwa sababu tafiti ambazo zilihusu futuhi, ziliegemea futuhi katika vitabu vya riwaya na tamthilia na hazikujikita katika suala la afya ya akili. Hivyo basi, makala haya yalinuia kujaza pengo hili kwa kutafitia futuhitandao na afya ya akili miongoni mwa Wakenya, na hasa kwa kuzingatia futuhi zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebook, Twitter na YouTube. Makala haya yalitumia nadharia ya Burudiko ya Sigmund Freud. Utafiti huu ulitumia muundo wa kiethnografia, mkabala wa kithamano. Data kuhusu futuhitandao ilikusanywa kwa mbinu ya Uchanganuzi wa Yaliyomo. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimakusudi na kinasibu. Umuhimu wa makala haya ni kuwa, matokeo yake yatasaidia katika ufundishaji wa futuhi. Inapendekezwa kuwa tafiti zaidi zifanywe kuhusu suala la afya ya akili kwa kurejelea vipera vingine vya fasihi simulizi.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini kenya
    (Eanso, 2019-08-23) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, Deborah
    Utafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji na uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu hasa ulilenga kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kudhihirisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundishia uainishaji wa nyimbo darasani na kuonesha namna ambavyo uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki huzisaidia nyimbo husika kutekeleza wajibu wake. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ufundishaji wa fasihi simulizi lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake unakanganya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu inayoonesha utaratibu wa kuainisha fasihi katika misingi ya aina mbalimbali kwa kuegemea miundo na maumbo, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii ambayo inashikilia kuwa ujifunzaji ni mchakato wa utambuzi ambao hujitokeza katika muktadha wa kijamii. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya. Kauli mbiu yake ilikuwa kuboresha umoja wa kitaifa kwa kuunganisha na kuleta watu pamoja. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu na ya kimakusudi. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano na picha. Mtafiti alipata kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulibaini kuwa, tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi darasani. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wana
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya
    (Easo, 2019-08-23) Magambo, Emilly Angushi; Simiyu, Fred Wanjala; Amukowa, Deborah
    Utafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji na uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu hasa ulilenga kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kudhihirisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundishia uainishaji wa nyimbo darasani na kuonesha namna ambavyo uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki huzisaidia nyimbo husika kutekeleza wajibu wake. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ufundishaji wa fasihi simulizi lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake unakanganya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu inayoonesha utaratibu wa kuainisha fasihi katika misingi ya aina mbalimbali kwa kuegemea miundo na maumbo, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii ambayo inashikilia kuwa ujifunzaji ni mchakato wa utambuzi ambao hujitokeza katika muktadha wa kijamii. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya. Kauli mbiu yake ilikuwa kuboresha umoja wa kitaifa kwa kuunganisha na kuleta watu pamoja. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu na ya kimakusudi. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano na picha. Mtafiti alipata kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulibaini kuwa, tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi darasani. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wanafunzi na walimu katika ufundishaji wa nyimbo kama kipera cha fasihi simulizi.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback