Browsing by Author "Adero, Margan"
Now showing 1 - 3 of 3
- Results Per Page
- Sort Options
Item Dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa wanandi(Easo, 2019-11-15) Koech, Jenniffer Chepleting; Simiyu, Fred Wanjala; Adero, MarganWakenya wengi hushutumu suala la umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za wasanii maarufu nchini. Madai yao ni kuwa umahuluti wa utamaduni husababisha kupotea kwa utamaduni asili wa jamii mbalimbali za Wakenya na kuiga ule wa Wakoloni. Utafiti huu ulikusudia kuhakiki dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wanandi nchini Kenya. Nadharia ambayo iliongoza utafiti huu ni ya ubaada ukoloni. Baadhi ya wahasisi wakuu wa nadharia hii ni Homi Bhabha, Gayatri Chakravorty Spinak, Edward Said, Robert Young na Bill Ashcroft. Mtafiti alipata data yake kupitia usaili na uchanganuzi wa yaliyomo kwenye vipindi vya Tumdo katika runinga ya Kass. Jumla ya wahojiwa nane walisailiwa kutoka kata ya Chepsaita, eneo la kaunti ndogo ya Turbo kwenye kaunti ya Uasin-Gishu. Idadi kubwa ya wakazi wa Uasin-Gishu ni Wanandi ambao walihamia eneo hilo kutoka kaunti ya Nandi; kwa hivyo wameingiliana na jamii zingine wa hapa nchini na kimataifa. Sampuli tajwa ilitumiwa kuteua wasailiwa. Nadharia ya ubaada ukoloni iliwaongoza mtafiti kubainisha vipengele vya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi. Hatimaye data iliyokusanywa iliwasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa: Nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kwenye runinga ya Kass zina vipengele vingi vya utamaduni wa jadi katika jamii ya Wanandi. Vilevile, nyimbo hizo zina baadhi ya vipengele vigeni hasa vinavyochangiwa na teknolojia na mwingiliano baina ya Wanandi na jamii zingine. Kadhalika umahuluti wa utamaduni umesaidia nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kutekeleza majukumu yake katika jamii ya sasa. Kwa hivyo, utafiti huu ni muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi na vyombo vya habari hasa kwa wale walimu na wanafunzi watakaotaka kufanya utafiti wa suala la dhima ya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi kwenye jamii za kiafrika.Item Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka(East African Journal of Swahili Studies, 2020-07-15) Chepkwony, Joyce; Simiyu, Fred Wanjala; Adero, MarganUtafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo. Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo. Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka. Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972. Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga. Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini. Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School. Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70. Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa. Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.Item Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka(KIBU, 2020-07-15) Simiyu, Fred Wanjala; Adero, Margan; Chepkwony, JoyceUtafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo. Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo. Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka. Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972. Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga. Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini. Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School. Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70. Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa. Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.
