Show simple item record

dc.contributor.authorAngushi, Magambo Emilly
dc.date.accessioned2019-11-26T13:55:43Z
dc.date.available2019-11-26T13:55:43Z
dc.date.issued2019-11
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/1858
dc.description.abstractWizara ya Elimu imekuwa ikitumia tamasha za muziki kuwaelimisha wanafunzi na hadhira kuhusu masuala mbalimbali. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu kipera cha nyimbo, lakini kuna haja ya kuchunguza njia mbadala za ufundishaji wa kipera cha nyimbo kwa sababu ni kipana mno na hata uainishaji wake hukanganya. Utafiti huu ulichunguza mchango wa tamasha za muziki kwa ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa: kupambanua uainishaji wa nyimbo katika tamasha za muziki, kubainisha namna uainishaji huu unavyoweza kutumiwa kufundisha uainishaji wa nyimbo darasani na kudhihirisha dhima ya nyimbo kupitia tamasha za muziki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu, mhimili wa pili unaosema kuwa, tanzu huleta muwala katika matini na kufanya kazi ieleweke kwa urahisi, pamoja na nadharia ya ujifunzaji kijamii, mhimili wa tatu unaoshadidia kuwa ujifunzaji hushirikisha utazamaji. Sampuli iliyolengwa katika utafiti huu ilijumuisha shule zilizoshiriki katika mashindano ya tamasha za muziki ya Kanda la Magharibi zilizofanyika mwaka wa 2018. Utafiti huu ulifanywa kwenye mashindano ya tamasha za muziki kiwango cha kikanda eneo la Magharibi yaliyofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Chavakali iliyo katika Kaunti ya Vihiga ambayo kauli mbiu yake ilikuwa “Kuboresha umoja wa nchi, utangamano na uelewano kupitia tamasha za muziki nchini Kenya.” jambo ambalo lilijitokeza katika uchanganuzi wa data ya utafiti huu hasa kupitia lengo la tatu lililoshughulikia dhima ya nyimbo kupitia tamasha za muziki. Watafitiwa ishirini na tano walihojiwa; wanafunzi 20 na walimu 5 walioteuliwa kinasibu. Mbinu ya kuteua sampuli ilikuwa ya kinasibu. Mbinu hii ya kinasibu ilitumiwa katika kuteua nyimbo 10 zilizotumika katika utafiti huu. Mtafiti alitumia utazamaji na mahojiano kama mbinu za kukusanya data. Data ilikuwa ya kithamano. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia maelezo ya kiufafanuzi na kuwasilishwa kwa maandishi yaliyoambatana na mifano ya nyimbo na picha. Utafiti ulibaini kwamba nyimbo zimeainishwa katika madaraja mbalimbali kutegemea vigezo kama vile umri, mahali na maudhui. Utafiti huu ulidhihirisha kuwa tamasha za muziki zinaweza kuwa njia mbadala ya kufundishia uainishaji wa kipera cha nyimbo katika shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu unapendekeza tamasha za muziki zichukuliwe kama mbinu nyingineyo ya kufundishia fasihi simulizi katika shule za upili. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa matokeo yake yataweza kuwafaidi wanafunzi na walimu katika ujifunzaji na ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo kama kipera cha fasihi simulizi tunapotilia maanani mtaala mpya unaohimiza umuhimu wa kuendeleza ujuzi na maarifa na pia kuzingatia maarifa hayo katika hali halisi za maisha.en_US
dc.language.isoSwahilien_US
dc.publisherKIBUen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.titleMchango wa tamasha za muziki katika ufundishaji wa uainishaji wa nyimbo katika shule za upili nchini kenyaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States