Show simple item record

dc.contributor.authorMukoya, Hillary Mauka
dc.date.accessioned2019-11-26T13:48:59Z
dc.date.available2019-11-26T13:48:59Z
dc.date.issued2019-11
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/1857
dc.description.abstractTafiti nyingi zimefanywa kuhusu utanzu mmoja kutumika kuwasilisha mawazo katika utanzu mwingine. Mbinu ya mwelekeo mseto imetafitiwa na wataalam mbalimbali kuhusu isimu kutumika kufundisha fasihi na fasihi kutumika kufundisha isimu. Hata hivyo, mtafiti hajakumbana na utafiti unaohusu utanzu mmoja wa fasihi kutumika kufundisha utanzu mwingine wa fasihi, hasa tamthilia kufundisha ushairi. Kumbe dhana ya usetaji inaweza kutumika katika ufundishaji wa tanzu za fasihi. Kwa hivyo, kuna haja ya kufanya utafiti kuhusu ufundishaji wa ushairi kwa kutumia tamthilia. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza namna tamthilia inavyotumika kufundisha ushairi katika shule za upili zilizoko Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini, Busia Kenya. Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa: kuchunguza namna ushairi unavyofundishwa katika shule za upili, kupambanua namna tamthilia inavyoweza kutumika kufundisha ushairi na kueleza mchango wa matumizi ya tamthilia katika ufundishaji wa ushairi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu ambayo iliasisiwa na Boas (1940) na kuendelezwa naye Bakhtin (1981). Nadharia hii ina mihimili ifuatayo: Mhimili wa kwanza unaoshikilia kuwa, tanzu huibua muundo wa kazi fulani ya fasihi na kufanya kazi hiyo ieleweke kwa urahisi sana; mhimili wa pili unaeleza kuwa, matumizi ya utanzu mwingine huwafanya wasomaji au wapokezi kuwa na ilhamu zaidi kuliko kuwapa kila wanachotarajia na mhimili wa tatu unashikilia kuwa, tanzu mbili zilizozoeleka zitumike kwa pamoja kwa sababu ya sifa zenye uhusiano mkubwa. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo. Sampuli ya utabakishaji wa kimakusudi ilitumika kuchagua shule za upili tisa (9) zilizowakilisha asilimia thelathini (30%) ya shule zilizo katika Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini iliyo na jumla ya shule thelathini (30). Kwa upande mwingine, sampuli ya kimakusudi ilitumika kuchagua mwalimu mmoja kutoka katika kila shule aliyeshiriki katika utafiti huu. Mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni usaili na uchunzaji. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia malengo mahususi ya utafiti. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa, vipengee vya mtindo, muundo na maudhui katika ushairi vilifundishwa kwa kutumia mbinu tofautitofauti za ufundishaji. Aidha, ilibainika kuwa, tamthilia ya Kifo Kisimani, Mstahiki Meya na Kigogo zilikuwa katika nafasi nzuri ya kufundishia mtindo, muundo na maudhui kwa sababu zilikuwa na bahari mbalimbali za ushairi. Mchango wa matumizi ya tamthilia katika ufundishaji wa ushairi ulionyeshwa; utafiti ulibaini kuwa, ufundishaji wa tamathali za usemi ulifanywa kwa urahisi, muundo wa ushairi ulifafanuliwa vizuri, wanafunzi walielewa maudhui kwa urahisi, walimu walikamilisha silabasi mapema, wanafunzi walichangamkia somo, ilhamu ya kutafiti iliibuliwa miongoni mwa wanafunzi na wanafunzi walimakinika darasani. Utafiti huu unapendekeza kuwa, walimu watilie maanani mbinu mahususi za ufundishaji wanapofundisha vipengee vya ushairi kama vile mtindo, muundo na maudhui ili kuhakikisha kwamba, wanafunzi wanafurahia utanzu wa ushairi. Vilevile, unapendekeza kuwa, usetaji katika ufundishaji na ujifunzaji uweze kutiliwa maanani na walimu wanapofunza ushairi wa Kiswahili kwa kusudi la kuondoa uchovu miongoni mwa wanafunzi. Aidha, unapendekeza walimu waboreshe mwelekeo wa ufundishaji mseto kusudi mada zinazofundishwa zieleweke bora zaidi. Pia unapendekeza kwamba, walimu wazingatie mchango wa matumizi ya tamthilia katika ufundishaji wa ushairi. Utafiti huu utawasaidia walimu wa shule za upili kuboresha zaidi ufundishaji wa ushairi kwa kuzingatia mbinu mahususi za ufundishaji wa ushairi. Utafiti huu pia utabainisha mchango wa kutumia tamthilia katika ufundishaji wa ushairi na hivyo basi, kufaa asasi zinazowaandaa walimu katika matumizi ya mbinu ya mwelekeo mseto katika ufundishaji wa fasihi.en_US
dc.language.isoSwahilien_US
dc.publisherKIBUen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.titleUfundishaji wa ushairi kwa kutumia tamthilia katika shule za upili nchini kenya: uchunguzi kifani wa kaunti ndogo ya teso kaskazinien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States