Show simple item record

dc.contributor.authorMohochi, Ernest Sangai
dc.date.accessioned2019-06-06T08:57:14Z
dc.date.available2019-06-06T08:57:14Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/1159
dc.description.abstractLugha ya Kiswahili imeenea na kukua kiasi cha kuweza kupambana na zingine katika ngazi za kimataifa kwenye mfumo wa sasa wa utandawazi. Hata hivyo, Kiswahili hakiwezi kupata fanaka inayotarajiwa huko nje iwapo hakithaminiwi na kudhaminiwa nyumbani (Afrika Mashariki). Bado lugha ya Kiswahili inakumbana na pingamizi nyingi mno; na miongoni mwa vikwazo hivyo ni mielekeo ya lugha inayobainika katika jamii. Makala hii inajikita zaidi katika mielekeo ya viongozi wa Afrika Mashariki, na wasomi wa Kiswahili kuhusu nafasi na umuhimu wa Kiswahili. Viongozi na wasomi wana ushawishi mkubwa sana kutokana na nafasi yao katika jamii. Wote wanaheshimika na kuenziwa; viongozi kutokana na mamlaka waliyopewa, na wasomi kwa sababu ya maarifa waliyonayo. Kutokana na ukweli huo, tabia na mienendo yao, pamoja na matamko yao mbalimbali yana athari kubwa sana katika jamii. Mara nyingi, watu wengi hupenda kuiga wayafanyayo; hali inayobainika pia katika matumizi ya lugha. Kabla ya kuijadili mielekeo na matumizi yao ya lugha, maswala mawili muhimu yanayochangia ujenzi wa hiyo mielekeo katika jamii yatazungumziwa: thamani ya lugha, na zoezi la kujifunza lugha ya pili.en_US
dc.language.isoSwahilien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.titleMielekeo ya wasomi wa kiswahili na viongozi wa Afrika mashariki kuhusu lugha ya kiswahilien_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States