Mielekeo ya wasomi wa kiswahili na viongozi wa Afrika mashariki kuhusu lugha ya kiswahili
Abstract
Lugha ya Kiswahili imeenea na kukua kiasi cha kuweza kupambana na zingine katika ngazi
za kimataifa kwenye mfumo wa sasa wa utandawazi. Hata hivyo, Kiswahili hakiwezi kupata
fanaka inayotarajiwa huko nje iwapo hakithaminiwi na kudhaminiwa nyumbani (Afrika
Mashariki). Bado lugha ya Kiswahili inakumbana na pingamizi nyingi mno; na miongoni
mwa vikwazo hivyo ni mielekeo ya lugha inayobainika katika jamii. Makala hii inajikita zaidi
katika mielekeo ya viongozi wa Afrika Mashariki, na wasomi wa Kiswahili kuhusu nafasi na
umuhimu wa Kiswahili. Viongozi na wasomi wana ushawishi mkubwa sana kutokana na
nafasi yao katika jamii. Wote wanaheshimika na kuenziwa; viongozi kutokana na mamlaka
waliyopewa, na wasomi kwa sababu ya maarifa waliyonayo. Kutokana na ukweli huo, tabia
na mienendo yao, pamoja na matamko yao mbalimbali yana athari kubwa sana katika jamii.
Mara nyingi, watu wengi hupenda kuiga wayafanyayo; hali inayobainika pia katika matumizi
ya lugha. Kabla ya kuijadili mielekeo na matumizi yao ya lugha, maswala mawili muhimu
yanayochangia ujenzi wa hiyo mielekeo katika jamii yatazungumziwa: thamani ya lugha, na
zoezi la kujifunza lugha ya pili.
Collections
The following license files are associated with this item: