Show simple item record

dc.contributor.authorSimiyu, Fred Wanjala
dc.contributor.authorWekesa, Winnie Musailo
dc.contributor.authorOpande, Nilson Isaac
dc.date.accessioned2021-03-12T06:51:31Z
dc.date.available2021-03-12T06:51:31Z
dc.date.issued2020-12-01
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/2324
dc.description.abstractUtafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.en_US
dc.language.isoSwahilien_US
dc.publisherKIBUen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.subjectNafasien_US
dc.subjectFasihi Simulizien_US
dc.subjectKisheriaen_US
dc.subjectUjumbeen_US
dc.titleNafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusuen_US
dc.typeOtheren_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States