Show simple item record

dc.contributor.authorKoech, Jenniffer Chepleting
dc.contributor.authorSimiyu, Fred Wanjala
dc.contributor.authorAdero, Margan
dc.date.accessioned2019-11-19T09:00:42Z
dc.date.available2019-11-19T09:00:42Z
dc.date.issued2019-11-15
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/1851
dc.description.abstractWakenya wengi hushutumu suala la umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za wasanii maarufu nchini. Madai yao ni kuwa umahuluti wa utamaduni husababisha kupotea kwa utamaduni asili wa jamii mbalimbali za Wakenya na kuiga ule wa Wakoloni. Utafiti huu ulikusudia kuhakiki dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wanandi nchini Kenya. Nadharia ambayo iliongoza utafiti huu ni ya ubaada ukoloni. Baadhi ya wahasisi wakuu wa nadharia hii ni Homi Bhabha, Gayatri Chakravorty Spinak, Edward Said, Robert Young na Bill Ashcroft. Mtafiti alipata data yake kupitia usaili na uchanganuzi wa yaliyomo kwenye vipindi vya Tumdo katika runinga ya Kass. Jumla ya wahojiwa nane walisailiwa kutoka kata ya Chepsaita, eneo la kaunti ndogo ya Turbo kwenye kaunti ya Uasin-Gishu. Idadi kubwa ya wakazi wa Uasin-Gishu ni Wanandi ambao walihamia eneo hilo kutoka kaunti ya Nandi; kwa hivyo wameingiliana na jamii zingine wa hapa nchini na kimataifa. Sampuli tajwa ilitumiwa kuteua wasailiwa. Nadharia ya ubaada ukoloni iliwaongoza mtafiti kubainisha vipengele vya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi. Hatimaye data iliyokusanywa iliwasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa: Nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kwenye runinga ya Kass zina vipengele vingi vya utamaduni wa jadi katika jamii ya Wanandi. Vilevile, nyimbo hizo zina baadhi ya vipengele vigeni hasa vinavyochangiwa na teknolojia na mwingiliano baina ya Wanandi na jamii zingine. Kadhalika umahuluti wa utamaduni umesaidia nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kutekeleza majukumu yake katika jamii ya sasa. Kwa hivyo, utafiti huu ni muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi na vyombo vya habari hasa kwa wale walimu na wanafunzi watakaotaka kufanya utafiti wa suala la dhima ya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi kwenye jamii za kiafrika.en_US
dc.language.isoSwahilien_US
dc.publisherEasoen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.subjectUmahulutien_US
dc.subjectUtamadunien_US
dc.subjectUamilishajien_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectTumdoen_US
dc.titleDhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa wanandien_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States