Kisima Chenye Hekima na Hadithi Nyingine

No Thumbnail Available

Date

2026-03-13

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Tunu Publishers

Abstract

Mkusanyiko huu ni wa kipekee maanake ni wa kwanza kufanywa na chama cha kitaaluma cha CHAKITA. Hivyo basi, ni kazi ambayo inagusa kina cha roho za wapenzi wote wa lugha hii adhimu ambao ni wanachama. Diwani hii ni ya kwanza katika mchakato mkubwa unaotarajiwa. Kufikia sasa, uandishi wa hadithi fupi umepevuka sana nchini Kenya na kwa wakati huu unashindana na riwaya na labda unapiku uandishi wa tamthilia ambao ni haba. Siyo kwamba tamthilia haziandikwi, la! Zipo tu ingawa hazichapishwi kwa wingi. Muhimu zaidi ni kuhusu toni mbalimbali ambazo tunazishuhudia katika utunzi wa hadithi fupi. Baadhi ya toni hizi ni kero, usisimuzi wa fikra, uchochezi wa hatua mwafaka na hata huzuni. Toni hizi zunatumiwa kuibua masuala mtambuko katika jamii. Pia ikumbukwe kwamba, kipengele hiki cha kimtindo kimechangamkiwa sana na waandishi wa hadithi fupi hivi karibuni.

Description

Book

Keywords

Diwani, Kisima chenye Hekima na Hadithi Nyingine, Tanabui la maisha, mchuuzi, Daftari la dadangu

Citation

Simiyu, F. C. N. W. & Leo, L. S. (2026). Kisima Chenye Hekima na Hadithi Nyingine. Nairobi, Kenya: Tunu Publishers.

Collections