Kufaa Kwa Nadharia Ya Uchanganuzi Vijenzi Katika Uchambuzi Wa Hiponimia
No Thumbnail Available
Date
2014-03-09
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kiswahili
Abstract
Hiponimia ni mojawapo ya mahusiano ya kifahiwa inayoashiria uhusiano ambapo leksimu ya
jumla inajumuisha kimaana leksimu mahususi. Uhusiano wa leksimu kihiponimia ulidhukuriwa
kuwa unafanana katika lugha anuwai ulimwenguni na aghalabu Hunahusisha leksimu nomino pekee.
Hata hivyo, tafiti za hivi punde zinadhihirisha kuwa hiponimia huonekana pia miongoni mwa
vivumishi, vielezi na vitenzi na huweza kutofautiana kimuundo na kimtindo kutoka lugha moja hadi
nyingine kwa sababu ya tofauti za kitamaduni. Wataalamu anuwai wamekuwa na mapendekezo
kadha kuhusu nadharia ifaayo ya kuainisha leksimu za lugha kihiponimia. Wengine wanaelekea
kupendelea matumizi ya nadharia ya Kiini Maana (Core Meanings Theory) na Nadharia ya
Sampuli Kifani (Prototype Theory). Hata hivyo inadhihirika kuwa nadharia ya Uchanganuzi
Vijenzi (Componential Analysis) inafaa zaidi katika uchanganuzi wa hiponimia ya leksimu nomino,
vitenzi, vivumishi na vielezi. Makala haya yanaangazia kufaa kwa nadharia hii katika uhakiki wa
hiponimia ikilinganishwa na nadharia Kiini Maana na Sampuli Kifani
Description
Journal Article
Keywords
Kiini Maana, Sampuli Kifani, Hiponimia, Uchanganuzi vijenzi
Citation
Okal, B. O., Indede, F., & Mohochi, E. S. (2016). Kufaa Kwa Nadharia Ya Uchanganuzi Vijenzi Katika Uchambuzi Wa Hiponimia. Kiswahili, 77, 85-103.
