Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria

Loading...
Thumbnail Image

Date

2020-08-13

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

KIBU

Abstract

Utafiti ulilenga kubainisha vipengele maalum vya Fasihi Simulizi vinavyooana na hali katika taaluma ya Sheria. Utafiti uliegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano ya utafiti. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha michakato miwili ya uteuzi wa sampuli; ikiwa ni uteuzi sampuli kimaksudi na kinasibu. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tulioyahudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaji kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.

Description

Keywords

Vipengele, Fasihi Simulizi, Taaluma, Sheria

Citation