Show simple item record

dc.contributor.authorMisiko, David Wasike
dc.date.accessioned2019-11-19T08:17:19Z
dc.date.available2019-11-19T08:17:19Z
dc.date.issued2017-01-12
dc.identifier.urihttp://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/1849
dc.description.abstractMatumizi ya lugha za kiasili yameshutumiwa na watu wengi kwa kukuza ukabila haswa nchini Kenya. Hata hivyo, lugha hizi zinaweza kuwa rasilimali kwa wazungumzaji zikitumiwa vyema. Utafiti huu ulilenga kuchunguza lugha za kiasili zinavyojitokeza kama rasilimali kwa wazungumzaji wake zinapotumika katika redio za FM. Aidha, utafiti ulinuia kujadili jinsi matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yanavyowezesha jamii husika kupata habari zinazoziwezesha kuboresha hali zao za maisha kwa njia mbalimbali. Uchunguzi ulidhamiria hususan: Kuhakiki yaliyomo katika vipindi vya jamii, uchumi, siasa na afya vinavyowasilishwa kwa kutumia Kibukusu katika redio za FM, zinazosikika katika kaunti ya Bungoma; Kutathmini Kibukusu kinavyojitokeza kama rasilimali kuangazia masuala ya jamii, uchumi, siasa na afya kwa wazungumzaji wake kinapotumika katika redio za FM, kisha kutambua changamoto za matumizi ya Kibukusu kama rasilimali kwa wakaazi wa Bungoma kupitia vituo vya redio za FM. Utafiti ulitumia mbinu za ustahilivu na kikiasi. Lahaja ya Kibukusu ilitafitiwa katika mazingira halisi ambapo lugha hiyo hutumika na wazungumzaji wake. Miktadha ya matumizi ya Kibukusu ilichunguzwa, hususan kama rasilimali kwa wazungumzaji wake. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili; Sarufi Amilifu ya Halliday na ya Uanzilishi wa Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Show. Sarufi Amilifu ilihusishwa katika uchanganuzi wa vipindi vinavyopeperushwa kwa kutumia lugha za kiasili. Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa vipindi vinavyopeperushwa na vituo hivyo viwili vya redio. Uchunguzi ulifanywa katika vituo vya Sulwe na West FM vinavyopeperusha matangazo kwa Kibukusu katika kaunti ya Bungoma. Utafiti ulihusisha mhariri mmoja, watangazaji wawili na wataalamu wanne; mmoja kwa kila mojawapo ya masuala haya; jamii, uchumi, afya na siasa ambao hualikwa kwa kila mojawapo ya vituo hivyo. Vilevile, wasikilizaji 70 kutoka kila mojawapo ya vituo hivyo viwili vya redio walihusishwa. Kwa jumla, utafiti uliwahusisha watu 154. Wasikilizaji hao waliteuliwa kutoka kwa kaunti ndogo sita za kaunti ya Bungoma na walihusisha jinsia zote. Wasikilizaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimakusudi ambao huwezesha idadi ya wahojiwa kuongezeka kadiri utafiti unavyoendelea. Vipindi vya redio vya vituo vyote viwili vilivyohusiana na masuala ya jamii, afya, uchumi na siasa vilisikilizwa. Mbinu ya ujazaji wa hojaji kwa watangazaji na wasikilizaji, usaili wa wahariri, watangazaji na wataalamu na kurekodi vipindi mahususi zilitumika. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa wanahabari, hohaji kwa wasikilizaji, mwongozo wa usaili kwa wahariri, watangazaji na wataalamu na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sarufi Amilifu. Data ifuatayo ilikusanywa: vipindi vya redio vinavyotumia lahaja ya Kibukusu, yaliyomo katika vipindi hivyo, Kibukusu kinavyojitokeza kama rasilimali kwa wazungumzaji wake na changamoto za matumizi ya lahaja hiyo katika redio za FM. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kwa maelezo na takwimu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa yafuatayo: Matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yalijaza pengo liliokuwepo katika upashaji habari kwa watu walioko mashinani; Matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM yaliwezesha wazungumzaji kufikia maamuzi faafu kuhusiana na masuala ya afya, siasa, uchumi na jamii; ukosefu wa taasisi ya kudhibiti uundaji wa istilahi ni mojawapo ya changamoto zinazokumba matumizi ya lugha za kiasili katika redio za FM. Matokeo ya utafiti huu yalitoa picha halisi ya mchango wa lugha za kiasili katika redio za FM nchini Kenya kwa maendeleo ya jamii husika. Matokeo ya uchunguzi huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu matumizi ya lugha za Kiafrika katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utawafaidi wapangaji lugha kitaifa na katika viwango vya kaunti. Utafiti huu pia unatarajiwa kutoa mchango kwa uhifadhi na makuzi ya lugha za Kiafrika kichanya. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Kuundwa kwa taasisi za kutafiti, kuunda na kudhibiti istilahi zinazotumika katika lugha za kiasili; Vyuo vikuu kufundisha baadhi ya lugha hizi za kiasili ili kubadilisha mtazamo hasi kuzihusu; Serikali za kaunti kuanzisha sera za lugha katika viwango vya kaunti na hatimaye, kufufuliwa kwa ufundishaji wa lugha za kiasili mbali na Kiingereza, Kiswahili na lugha zingine za kigeni kama vile Kifaransa na Kijerumani katika sera ya lugha nchini Kenya.en_US
dc.language.isoSwahilien_US
dc.publisherMoi Universityen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/3.0/us/*
dc.titleLugha kama rasilimali ya jamii: uchunguzi wa redio za fm zinazotumia kibukusu katika kaunti ya bungomaen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 United States